Posts

Showing posts from February 6, 2018

DR.SLAA: SIKUWAHI KUSEMA NIMEACHA SIASA.

Image
Katibu mkuu wa zamani chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na balozi mteuli awamu ya tano, Dr. Wilbroad Slaa amesema kuwa hakuwahi kusema ameacha siasa bali alisema ameacha siasa za vyama vingi. Kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na runinga ya Clouds Media Group (CMG), leo jumanne Februari 2018, Dr. Slaa amesikika akiyasema hayo na kuongezea kuwa kutokuwa na chama haimanishi ameacha siasa. “Skuwahi kusema nimecha siasa na kama kuna mtu alikuwepo kwenye mkutano wangu pale Serena Hotel nilisema naachana na siasa za vyama vingi, na sina chama lakini haimanishi nimeacha siasa” Dr. Slaa. Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, amesema kila mtu ana mapungufu yake kwa wagombea waliokuwepo ila Magufuli ana afadhali. Pia amesema Bunge ni maazimio na huleta maana pale mijadala inapopigiwa kura na kuongeza kuwa bungeni sio kuongea kwa ukali. Akijibu swali aliloulizwa kuhusu kukimbilia Canada amesema kuwa ni nchi ambayo ina rekodi nzuri ya haki za b

CUF yamtaka Diwani wao kuacha kuandamana na mgombea wa Chadema

Image
Dar es Salaam. Katibu wa CUF  Ally Mkandu amemtaka Diwani wa kata ya mzimuni Ally Kondo kuacha kuongozana na mgombea wa Chadema Salum Mwalimu. Amesema kwamba diwani huo asipoacha kuongozana na mgombea huyo chama kitamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutumia katiba kumvua uanachama. Amesema hayo leo Februari 5 wakati akimnadi mgombea Ubunge  wa Kinondoni Rajabu Salum. Mkurugenzi wa Habari na uenezi Abduli Kambaya amewaambia wakazi wa mzimuni  kwamba mwaka 2015  CUF ilipata  ushindi kwa kufanya kazi kubwa kwenye kata ya mzimuni. ‘’Leo anajitokeza mtu anawashawishi mumchague mgombea mwingine  inauma sana’’amesema  Kambaya Naye mgombea  Rajabu Salum amesema kwamba ‘’Mimi nilikuwa meneja kampeni wa mgombea wa huyu aliyehamia  CCM( Maulid Mtulia)  hivyo mimi nilikuwa mwalimu wake’’ Amesema mgombea huyo sasa ameanza kutumia sera za Cuf  kwenye majukwaa. ‘’CCM na Chadema wameahidi kunipa kura kwa kuwa wagombea wao hawakushiriki kwenye kura za mao