TRA wavuka lengo kwa kukusanya Sh trilioni 1.3
Akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es salaam kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata amesema ongezeko la makusanyo linatokana na jitihada zinazofanyawa na TRA katika kuongeza kasi ya usimamizi wa ufuatiliaji na ukadiriaji wa kodi kwa usahihi. “Tumejitahidi kudhibiti biashara za magendo katika maeneo ya Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, mipakani na maziwa yote, Alisema Kamishna Mkuu. Amesema hadi kufikia Machi 2016, tayari TRA imekusanya shilingi Trilioni 9.89 sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya shilingi trilioni 9.99 mwaka wa fedha 2015/2016. Bw. Alphayo amewasisitiza wafanyabiashara ambao hawajasajili biashara zao kufanya hivyo mara moja kupitia ofisi za TRA zilizoko katika maeneo ya biashara zao na kwa wale wanaoshiriki vitendo vya uingizaji bidhaa za magendo nchini amemewata kuacha mara moja kwani vinaipotezea serikali mapato. “Wakikamatwa katika msako ...