Posts

Showing posts from May 23, 2013

MADAM RITHA WA BSS AELEZA JINSI ALIVYOPATA AJALI

Image
Kilichompata Madam Rita kinasikitisha! Ndivyo unavyoweza kusema ukibahatika kumuona the big boss wa Benchmark Production inayoratibu Shindano la Bongo Star Search , Rita Poulsen ‘Madam’ anayetembelea magongo baada ya kupata ajali mbaya ya gari. Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kuwa kimya muda mrefu ikielezwa kuwa alipata ajali hiyo kitambo, Madam Rita alisema kuwa kwanza kabisa anamshukuru Mungu kwani anaamini kila kitu kinachotokea chini ya jua kina sababu yake na hata alipopata ajali hiyo alimshukuru kwa kutoka salama.  Kabla ya ajali Madam Rita aliendelea kueleza kuwa ajali hiyo aliipata katikati ya Jiji la Dar  na kusababisha kuvunjika kwa kifundo ‘enka’ cha mguu wa kulia hivyo kumsababishia kutembelea magongo baada ya hospitali kumuwekea ‘hogo’. “Namshukuru Mungu kwanza kwa kunitoa salama katika ile ajali japokuwa sijapona vizuri,” alisema Madam Rita. Mkurugenzi huyo aliendelea kueleza kuwa alipopata ajali hiyo alikimbizwa katika...

BINTI ALIYETOROKEA UINGEREZA AKIMKWEPA MFALME MSWATI

Image
HUYU NDO BINTI ALIYETOROKEA UINGEREZA AKIKWEPA KUTOMASWA NA MFALME MSWATI Msichana mdogo ameomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza baada ya kukataa kwa dharau harakati za ndoa za wake wengi za Mfalme Mswati III wa Swaziland na kugoma kujiunga kwenye nyumba harimu ya wake 13. Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta hisia za mfalme huyo milionea, mtawala maarufu mkandamizaji kwa maisha yake ya anasa. Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme Mswati III, mwenye umri wa miaka 45, anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila mwaka.   Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini Birmingham, alikuwa na umri wa miaka 15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya harakati zake baada kumuona kwenye jumba la kifalme la mke wake wa nne, LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika' pale alipogundua dhamira zake za ndoa. Aliongeza: "Alianza kunipigia simu k...
Image
MSANII ELIZABETH 'LULU' MICHAEL KURUDI SHULE...!!! Elizabeth 'Lulu' Michael BAADA ya kupata dhamana msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ajipanga kujiendeleza na masomo ili aweza kupambana na changamoto za maisha. Akizungumza na Maisha msanii wa filamu ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu  familia ya Lulu Mahfudh Hussein 'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake Alisema kuwa ingawa familia ina mikakati hiyo suala kubwa linalokwamisha kwa sasa ni kipato kwani familia yake haina uwezo wa kumlipia msanii huyo na badala yake anatakiwa Lulu kuanza kufanya kazi ili aweze kujikwamua kwa hilo Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa kutokana na kipato cha familia ya msanii huyo hivyo anatakiwa kwa sasa aweze kufanya kazi ya filamu ili aweze kujimudu kama ilivyokuwa mwanzo na maisha yaendele "Hapo awali alikuwa na uwezo wa kuihudumia familia yake kwa njia ya...

SIMBA YASEMA KUONDOKA KWA NGASA HASUMBUI

Image
Simba:Ngasa hatusumbui kichwa Share bookmark Print Email Rating   Na Jessca Nangawe  ( email the author ) Posted  Jumatano,Mei22  2013  saa 9:27 AM Kwa ufupi Mwanzoni mwa wiki hii, Ngassa alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, klabu aliyoichezea kabla ya kujiunga na Azam FC na kisha kutua Simba alikocheza msimu mmoja uliomalizika wiki iliyopita  Baada ya siku mbili tu kupita tangu winga wa Simba, Mrisho Ngasa ajiunge Yanga, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage amesema kuondoka kwa mchezaji huyo hakuwasumbui hata kidogo. Mwanzoni mwa wiki hii, Ngassa alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, klabu aliyoichezea kabla ya kujiunga na Azam FC na kisha kutua Simba alikocheza msimu mmoja uliomalizika wiki iliyopita. Simba wanadai Ngassa alikuwa tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kwao, kabla ya kusaidi wa Yanga jambo linali...

NDOA YA DIAMOND PLATINUM NA PENNY YANUKIA

Image
NDOA YA DIAMOND PLATNUMZ NA PENNY YANUKIA. Maharusi watarajiwa Dimaond Platnumz & VJ Penny Esma Abdul ambae ni dada yake mwimbaji staa wa Tanzania, Diamond Platnums, amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae anatarajiwa kumuoa mtangazaji wa TV aitwae Penny. Esma ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, "Tumemkubali sana wifi yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye ataniingilia kwenye mapenzi yangu." Huu ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa. Dada yake Diamond aka wifi yake Penny Zaidi ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nch...

MWILI WA HAYATI CHINUA ACHEBE ULIVYOWASILI NCHINI NIGERIA

Image
HIVI NDIVYO MWILI WA HAYATI CHINUA ACHEBE, ULIVYOWASILI NIGERIA In the early hours of Tuesday May 21st, 2013, the corpse of late Prof. Chinua Achebe arrives the Federal Capital Terrorist ( Abuja ) ahead of his burial on Thursday. See more photos of the late Chinua Achebe’s casket below.

MATUKIO YA VURUGU MTWARA

Image
NYUMBA YA MWANDISHI WA HABARI WA TBC YACHOMWA MOTO HUKU MABOMU YAKIRINDIMA HUKO MTWARA Hali imezidi kuwa mbaya katika Mji wa Mtwara na hivi punde watu wanaendelea kufanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya mji huo. Jengo moja ambalo linadaiwa kumilikuwa na CCM limechomwa moto katika eneo la Majengo na daraja linalounganisha Lindi na Mtwara limevunjwa. Mbali na hayo pia nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC)imechomwa moto. Katika Mji wa Mtwara milio ya mabomu na risasi ndio inayosikika kila kona. Jeshi la Polisi linajaribu kuwadhibiti vijana  na watu wengine ambao wanafanya vurugu hizo.   VURUGU ZA MTWARA ZASABABISHA BUNGE LIAHIRISHWE.... Spika wa bunge , Anne Makinda ameahirisha Bunge kutokana na hali ya Mtwara na ameiagiza serikali kuwa kesho wawasilishe taarifa bungeni kuhusiana na hali hiyo. Makinda ameitisha kamati ya uongozi ili kuona kama wanaweza kutuma kamati ya Bunge kesho kwenda huko.

PROFESA J. AJIUNGA NA CHADEMA

Image
PROFESA JAY AJIUNGA NA CHADEMA TAYARI KWA KUENDELEZA MAPAMBANO YA KISIASA KAMA MKONGWE SUGU Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu.  Kujiunga rasmi kwa Profesa kwenye chama hicho kunaashiria kuwa huenda akawa na nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015. Profesa ameamua kuweka wazi uamuzi wake baada ya watu wengi kuanza kumuuliza maswali. “Mmeniuliza sana kwamba mimi ni CHAMA gani jibu litapatikana Muda sio mrefu!! Still in Dodoma STAY TUNED,” alitweet.   Rapper huyo anayejulikana kama mchawi wa rhymes yupo Dodoma pamoja na wasanii wengine akiwemo Lady Jaydee kwa mwaliko wa Sugu

SHEHA WA TOMONDO-ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI

Image
PICHA ZA SHEHA WA TOMONDO- ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI JANA USIKU \ Sheha Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole. Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua. Sheha Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo.
Image
Why Obama is coming to Tanzania Share Bookmark Print Email Rating President Barack Obama meets his Tanzanian counterpart Jakaya Kikwete in the Oval office at the Whie House. In his second tour of Africa next month Mr Obama will visit three African countries, which include Tanzania, Senegal and South Africa. PHOTO | FILE  By Elisha Magolanga  ( email the author ) Posted  Tuesday, May 21  2013 at  22:32 In Summary President Barack Obama will come with a delegation of more than 1200 people, including 500 businessmen and investors. He becomes the third US President to, consecutively, visit Tanzania after Bill Clinton in 2000, and George Bush in 2008. The US President’s tour of Africa will start on June 26 and end on July 3. In addition to Tanzania he will also visit Senegal and South Africa SHARE THIS ...