Rais JPM Uso kwa Uso na Lowassa
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa wakati wa hafla ya maadhimisho ya Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa . Kushoto ni Mama Regina Lowassa Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mhe. Edward Lowassa wakati wa ibada ya maadhimisho hayo. Rais Magufuli akiongea jambo na Mhe. Lowassa. Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa katika picha na Rais Magufuli na viongozi wastaafu na wana familia. Rais Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwapongeza Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa. Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipongezwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea zawadi kutoka Parokia ya Upanga...