LHRC: Wafungwa 470 Wanasubiri Kunyongwa
Dk. Kijo-Bisimba. WATU 472 waliohukumiwa adhabu ya kifo kutokana na makosa mbalimbali, wanasubiri saini ya Rais Dk. John Magufuli ili kujua hatima ya utekelezaji wa adhabu zao ama laa. Takwimu hizo zinaonesha kuwa kati ya watu hao, wanaume ni 452 na wanawake ni 20. Taarifa hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu adhabu ya kifo. Bisimba alisema, watu hao walihukumiwa adhabu ya kifo kutokana na kutiwa hatiani na makakama kwa makosa ya uhaini na mauji. Licha ya adhabu hiyo alisema hatua ya utekelezaji wake inakwenda kinyume na haki za binadamu kama inavyotafsiriwa katika matamko na mikataba mbalimbali ya kimataifa. Kutokana na hali hiyo, Dk. Kijo-Bisimba, alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa adhabu hiyo. Alisema wakati watu hao wakisubiri adhabu hiyo, wengine 244 waliopo katika magereza mbalimbali bado wanasubiria m...