Rais Magufuli: Bora Kula Sumu Kuliko Fedha za Serikali
Rais Magufuli leo Ijumaa ameweka jiwe la msingi la Barabara ya Kidatu – Ifakara. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Wabunge wote wa Chadema na CCM mkoani Morogoro. Moja ya kauli ambazo Rais amezungumza leo; “Kuna maeneo ambayo wakandarasi wamekula hela za miradi, wamekula sumu. Hela ya Serikali ya awamu ya tano hailiwi bora ule sumu kali. Waliokula fedha waanze kujiandaa, kurudisha fedha na kutekeleza miradi au kukumbana na sheria ya mwaka 97.” “Haiwezekani mimi nitafute hela halafu wewe uzile tu nikwambie umeula wa chuya. Kama makandarasi watakuwa wamekimbia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, polisi na Takukuru wawatafute popote. Watazitapika hizo fedha wanazozitafuna,” amesisitiza Rais. Amesema hatojali fisadi ametoka CCM, Chadema wala CUF au nje ya nchi, atawashughulikia. Mbunge wa Kilombero, Lijualikali(CHADEMA) “Ukiniambia leo uwape zawadi gani watu wa Morogoro maana kuna mengi lakini naomba watu wote ambao wamechukua ardhi yetu na hawaifanyii kazi basi naomb...