Mongela Atinga Mitaani Kuhimiza Usafi wa Jiji la Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akikatiza katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza kuhimiza usafi. Mhe. John Mongela akitoa maelezo kuondoa vitu vilivyowekwa nje ya duka la mkazi wa Mwanza. Wakazi wa Mwanza eneo la soko kuu wakiondoa uchafu katika mtaro uliopo eneo hilo. Mwananchi huyu akiondoa takataka zilizopo kwenye mtaro uliopakana na duka lake. Zoezi la kusafisha Jiji la Mwanza likiendelea. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ametembea mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza kuhimiza watu kufanya usafi katika maeneo wanayofanyia kazi pamoja na kutoa muongozo wa namna wafanyabiashara watakavyoendesha biashara zao. Ziara hiyo imefanyika baada ya kumaliza zoezi la kuondoa wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuwapeleka maeneo mbalimbali ambayo yalitengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao. Katika ziara hiyo iliyokuwa imeambatana na viongozi mbalimbali wa serikali walipita maeneo ya Makorobo...