HOT NEWS: WANANCHI WENYE HASIRA KALI WAMPIGA NA KISHA KUMCHOMA MOTO KIJANA MMOJA ALIYETUHUMIWA KUIBA NG'OMBE .
Mwili wa Kijana huyo Ukiwa umefunikwa na Majani Kabla ya Kuchomwa Moto Mwili wa Kijana huyo ukiwa unachomwa Moto na wananchi wa Eneo hilo Akielezea Tukio Lilivyo tokea Ng'ombe Walioibiwa Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo ********************** WAKATI vyombo mbali mbali zikiendelea na jitihada za kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi hali hiyo bado ni tete mkoani Mbeya. Hali hiyo imezidi kujitokeza baada ya Wananchi wenye hasira kali wa Mwasanga Ivumwe jijini Mbeya kumpiga na kumchoma moto mwananchi mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakimtuhumu kwa Wizi wa Ng’ombe mmoja na ndama. Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ameuambia mtandao huu kuwa tukio hilo lilitokea mapema leo asubuhi ambapo chanzo ni wizi wa Ng’ombe wa Kongoro Mwakitalima mkazi wa Isyesye kata ya Ilomba. Alisema Ng’ombe huyo aliibiwa jana majira ya usiku ambapo mzee huy...