Posts

Showing posts from March 14, 2018

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA ITAKAYOTUMIA UMEME SGR-KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA- DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali

Kauli ya Wakili wa viongozi mtandao wa wanafunzi

Image
Wakili wa viongozi wa  Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Reginald Martine amesema wateja wake wameitwa kuhojiwa na mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kutoa ushahidi wa tukio la ‘kutekwa’ kwa mwenyekiti wao, Abdul Nondo. Akizungumza na MCL Digital leo Machi 14, 2018, Martine amesema tayari viongozi wawili kati ya wanne wa mtandao huo wameshatoa ushahidi wao, kwamba hakuna vitisho vyovyote walivyopewa na polisi. Amesema kuwa polisi wamemhakikishia kuwa hawatawashikilia viongozi hao na mara watakapomaliza kutoa ushahidi wataruhusiwa kuondoka. “Utaratibu wa wakili mtu anapokuwa anatuhumiwa lazima uwe na mteja wako wakati anapohojiwa lakini kama mteja anatoa ushahidi wakili siyo lazima awepo hivyo wanaendelea kutoa ushahidi muda,” amesema. Amesema walishauriana na  mmoja wa makamishna kuwa yeye asiwepo na viongozi hao wakati wanatoa ushahidi wao. Waliofika kuhojiwa na  DCI ni mkaguzi wa haki za binadamu, Alphonce Lusako; katibu wa mtandao hu

Nyama kutoka Afrika Kusini yateketezwa na ZFDA

Image
Picha ya Mtandao Zanzibar. Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), imeteketeza  kilo 48 za nyama kutoka Afrika Kusini baada ya Serikali kusitisha uingizaji nyama kutoka nchini humo kutokana na mlipuko wa bakteria wa listeria. Ilibainika kuwa nyama hizo ziliingizwa nchini kinyume cha sheria, Nyama hizo ni mali ya kampuni ya Qamar ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, ilikamatwa Uwanja wa wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza leo Machi 14 wakati wa zoezi hilo, mkuu wa kitengo cha uchambuzi wa hatari zinazotokana na chakula wa ZFDA, Aisha Suleiman amesema kilichosababisha kuteketezwa kwa nyama hiyo ni katazo lililotolewa na ZFDA baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa wa listeriosis. Amesema ZFDA ndiyo yenye majukumu ya kuhakikisha wananchi wanapata chakula salama, Aisha amesema uamuzi ya katazo hilo umetokana na uwapo wa maradhi ya Listeriosis nchini Afrika Kusini, hivyo ofisi yao imepiga marufuku uingizwaji nyama, maziw

ANGALIA MAPOKEZI YA A BOY FROM TANDALE YA DIAMOND PLATINUMZ NCHINI KENYA

Image
Kwanza kabisa Diamond kafanya kitu kizuri kwa kuonesha ni kwa namana gani nchi hizi mbili zipo vizuri na kushirikiana vema si kama ambavyo watu wengine huleta ushirikiano wa maneno Sasa hivi Kenya na Tanzania wamekuwa ndugu kwa kuunganishwa na msanii wetu Diamond planumz. Kwa haraka haraka nimejaribu kupitia taarifa mbali mbali za kwenye media nikaona kenya wanampo support ya kutosha kijana wetu. Kwa pamoja tunapaswa kumsapot na kumpongeza kwa hatua hiyo na kwa ukalimu wa watu wa kenya wanao ufanya kwa ndugu yetu huyu.