Posts

Showing posts from October 12, 2017

Miili ya Wanajeshi wa JWTZ Waliouawa DRC Yaagwa

Image
Miili ya askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imeagwa tayari kwa kurejeshwa nchini. Askari hao walikuwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa (UN). Habari zilizopatikana zilisema miili ya askari hao iliagwa jana. JWTZ katika taarifa kwa umma juzi iliwataja askari hao kuwa ni Koplo Maselino Paschal Fubusi na Praiveti Venance Moses Chimboni. Taarifa ilisema askari wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na kundi la wapiganaji la ADF. Taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya JWTZ ilisema askari hao walishambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi Oktoba 9, wakiwa umbali wa kilomita 24 mashariki mwa mji wa Beni. JWTZ ilisema UN inaandaa utaratibu wa kuirejesha miili ya askari hao na utakapokamilisha wataujulisha umma mapokezi, kuaga na mazishi yatakavyokuwa. Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani mauaji hayo ya...

Hatari ya kuvalia viatu bila soksi

Image
               Ukivalia viatu vyako bila soksi unajiweka katika hatari ya makubwa zaidi kuliko kunuka kwa miguu pekee.Chuo cha tiba ya miguu nchini Uingereza kinasema karibuni kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya maradhi yanayosababishwa na kuvu kutokana na kuvuma kwa mtindo wa kuvalia viatu bila soksi, hasa miongoni mwa vijana.Mtaalamu Emma Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au kuvalia viatu visivyowatosha vyema.Kutovalia soksi siku hivi kumekuwa mtindo maarufu wa mavazi, na mwanamuziki Sam Smith ni miongoni mwa watu wanaojitokeza hadharani wakiwa na viatu bila soksi.                   Wanaume wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.Mwanamuziki Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara nyingi kati...

HAWA NDIO WANAOKULA MEME YA UTEANDAJI WA RAIS MAGUFULI

Image
         Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli watu wengi wamekuwa wakihoji ni nani hasa anayenufaika na huu utawala.. Malalamiko mengi yamekuwa yakitolewa na watetea mafisadi wa ufipa kwamba zama za Rais Magufuli kila mtu anaisoma namba wala hamna mwenye nafuu. Lakini uchunguzi niliofanya umenipa majibu tofauti kabisa. Watu wafuatao wanakula mema ya Rais Magufuli kwa sana tu na hawataki kabisa atoke madarakani. 1. Wamachinga Kabla ya Rais Magufuli kuwa machinga ilikuwa ni balaa tupu ,kila siku walichezea vipigo na kuchukuliwa bidhaa na mgambo. Leo ndani ya utawala wa Rais Magufuli wamachinga wanafanya biashara ndani ya jiji bila shida yoyote. Kwa nini wasimpende Magufuli? 2. Wakulima Chini ya utawala wa Rais Magufuli kodi zote za ajabu ajabu zimefutwa hivyo kuongeza tija kwa wakulima. Mazao ya chai ,korosho, Pamba, mpunga, tumbaku yalikuwa na kodi zaidi ya kumi!!! Sasa kwa nini wasimpende Rais Magufuli?? 3. Wafugaji K...

Nafasi za Kazi Standard Bank Tanzania

Image
Job Details Risk Management: understanding all risks – from the economic to the political – that could affect our global business, and offering guidance to all parts of the bank Job Purpose To asses information provided and consolidate in an Application for Facilities (AFF),  with focus on the need and structure of facilities, asses counter-party credit risks associated with the bank’s CIB lending and investment activities at the Business and client interface, with the primary objective to contain credit risk within acceptable parameters and in compliance with the Credit Policy and Product Parameters. Manager, Credit Originati Overview Job ID: 27802 Job Sector: Banking Closing Date: Oct 16 2017 Country: Tanzania Region/State/Province/District: Dar es Salaam Region Location: Dar es Salaam Key Responsibilities/Accountabilities Provision of direct (specialist/ professional) credit assessment services at the Business and  customer interface: Iden...

Nafasi za Kazi Mamlaka ya Reli Ya Tanzania na Zambia (TAZARA)

Image
The Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA) is a statutory institution owned by the two Governments of the United Republic of Tanzania and the Republic of Zambia on a 50/50 shareholding basis. Incorporated by the Acts of Parliament of the two contracting states, the Authority’s registered office is in Dar es Salaam, Tanzania, with two regional administrative centres in Mpika, Zambia and Dar es Salaam. Some positions have fallen vacant and, in this regard, applications are invited from suitably qualified applicants, as follows. Corporation Secretary-1 Position Reporting to: Managing Director Duty Station: Head Office Job Purpose To advise Management on legal matters and provide legal and administrative services to the Council of Ministers, Board of Directors and the Authority in general as well as safe guard Authority interests and asset utilisation. Main Duties a) Providing legal, administrative and secretarial services to the Board of Directors and Counc...

Waziri atoa miezi sita kwa wakuu wa shule

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa miezi sita kwa wakuu wa shule za msingi na sekondari nchini kuanzisha madawati ya ulinzi na usalama wa watoto kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wanafunzi. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike kitaifa iliyofanyika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara amewasisitiza wakuu wa shule za msingi na sekondari kuzingatia uwepo wa dawati la ulinzi na usalama wa mtoto kike katika shule zao ili kuwa salama na kuwa na mahali pa kueleza matatizo yao. Mh. Ummy ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila mmoja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa jitihada zao na kushirikiana na serikali kutoa elimu kwa wanajamii kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la kutokomeza ukeketaji Tarime Stela Mgaya amesema kuwa wamefanikisha kuwaondoa mangariba 63 kut...