NIMEUPOKEA UTEUZI..... Ndugu zangu, nimepokea majukumu niliyokabidhiwa na Baraza Kuu la chama changu. Siwezi kuepuka majukumu haya muhimu kwa wakati huu ambapo chama kinahitaji mchango wangu. Niko IMARA sana, natambua nimepewa majukumu wakati gani na nianze na mguu upi kwenda mbele. Uongozi ni MZIGO na si kazi nyepesi, nahitaji kusaidiwa, kushauriwa, kuombewa na kuungwa mkono na watu wenye nia njema na siasa za mabadiliko ya kweli hapa nchini, walio ndani na nje ya CUF. Natambua kuwa wapo wana CUF wenye sifa, uwezo, vigezo na busara kunishinda, lakini kwa sasa chama kimeona naweza kuuungana na wenzangu kukisimamia. Naahidi kuwa ntatoa uongozi wa KISASA wenye kushughulikia MASUALA. Ntatimiza wajibu wangu bila hofu yoyote kama kawaida yangu na ntatoa UONGOZI WA PAMOJA (Collective Leadership) kwa kila mwenye nia safi na CUF na mabadiliko. Nitakuwa mhimili imara katika kipindi hiki cha mpito, kuhakikisha CUF inafanya kazi zake na inaimarika ili kujenga uwezo wa ndani, k...