MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI KATI YA BASI LA MAJINJAH NA TOYOTA HILUX MBEYA
Gari aina ya Toyota Hilux ambayo imegongwa na Basi la Kampuni ya Majinja likiwa linatoka Mbeya kwenda Dar. (Picha na Fahari news) Mtu mmoja amefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamenusurika kifo katika ajali ya barabarani iliyotokea majira ya saa 12:15 asubuhi njia panda ya Mafiati jijini Mbeya ikihusisha magari mawili yaliyogongana uso kwa USO. Ajali hiyo imehusisha basi la abiria mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa likielekea Dar es Salaam kutoka jijini Mbeya na gari dogo ambalo halikufahamika Mara Moja. kutokana na kuharibika sana ambalo dereva wake amepoteza maisha pale pale na hakufahamika jina lake mara moja. Pamoja na hayo shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mlinzi katika kituo cha Oilcom Mafiati amesema kuwa dereva wa basi la Majinja ambaye hakufahamika kwa jina alikuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi kitu kilicho sababisha gari kumshinda na kuparamia gari do go lililokuwa likitokea Mwanjerwa na kuharibika kabisa. ...