BINTI ANALAZIMISHA NDOA ANATAKA KUNISAIDIA KUTOA MAHARI...NAOMBA USHAURI JAMANI
... Awali ya yote nina mwanamke mmoja ambaye tulianza naye mapenzi toka tuanze wote kazi kwa sababu tumeajiliwa sehemu moja ila tu tunatofautiana sehemu ya kufanyia kazi yeye anafanyia wilayani na mimi nafanyia mkoani sasa toka tuanze imefika kipindi akabeba ujauzito na saizi ni miezi mitano tangu abebe huo ujauzito sasa anataka nikatoe mahali kwao ili wanitambue wazazi wake rasmi yeye ndio mpanga mahali na anasema ni milioni moja mahali pamoja na masufuria ya shangazi na babu na branket la bibi. Mimi nikamwambia kuwa hicho kiasi sina akasema kuwa yeye atoe laki nne na mimi nimalizie laki sita na leo kanipigia simu kuwa inatakiwa ipelekwe barua ya kishika uchumba pamoja na elfu therathini mimi pia nikasema kuwa saizi sina hela yeye akasema kuwa mimi niandike barua atakuja kuichukua na ataituma nyumbani kwao kwa njia ya posta na ataiweka hiyo elfu therethini na kuituma nyumbani sasa ninachojiuliza ataka tuoane mapema ili amiliki baadhi ya vitu vyangu ...