MANSOUR AKATAA KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA UAMUZI WA KUFUKUZWA CCM
Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilisihi Jimbo la Kiembe Samaki (CCM) Mansour Yussuf Himid amesema licha ya kufukuzwa Uanachama katika chama hicho hatoenda Mahakamani kutetea nafasi hiyo kwani kufanya hivyo ni kukaribisha Malumbano ambayo hayana tija. Amesema kwenda kupinga uamuzi huo Mahakamani ni kuhalalisha yeye kuwa Mwakilishi wa Mahakama badala ya Wananchi jambo ambalo hapendelei kutokea katika maisha yake. Mansour ameyasema hayo leo katika Kongamano la Kamati ya Maridhiano lililofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. Amesema amekuwa akiulizwa Maswali mengi na Watu tofauti kuhusu mustakabali wake kisiasa baada ya kufukuzwa uanachama na kuongeza kuwa hana Pesa za kuchezea kwenda kupinga uamuzi wa Chama cha Mapinduzi Mahakamani. "Wenzangu wamenipima na wameniona sifai ni haki yao, siendi Mahakamani, sina pesa za kuchezea wala sitaki kuwa Mwakilishi wa Mahakama" Alisema Mansour. Mansour aliyejiung...