Rais Magufuli aibua mapya bandarini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Dkt. John Pombe Magufuli, leo amefanya ziara ya kushtukiza bandarini jijini Dar es salaam kukagua matanki ya mafuta ya kula, ambayo yameadimika hapa nchini. Baada ya ziara hiyo na kufanya ukaguzi, Rais Magufuli amebaini kuwa kuna mafuta ambayo yameingizwa nchini huku kukiwa na taarifa za udanganyifu ili kukwepa kodi, yakiwemo mafuta ambayo yameshakamilika (refined oil) na kusema kuwa ni mafuta gahfi (crude oil). Baada ya kugundua hilo Rais Magufuli amewataka wamiliki wa mafuta hayo kulipa ushuru wake unaostahili, pamoja na fine kutokana na udanganyifu walioufanya. "Kwenye bidhaa walizosema ni crude kumbe ni refined oil walipe 25% pamoja na fine, hatuwezi tukawa tunaibiwa kila siku tunahitaji kujenga viwanda vetu, haiwezekani crude oil ukachaji sawa na semi refined, na hii sheria yetu inawezekana kulifanyika mchezo, wabunge walipitisha kitu kingine, kinachojadiliwa kingine, kilicholetwa huku ni kingine, kinachokuja kupi...