Mkazi wa Mbezi-Kibanda, Andrea Marcus. AMA kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao, Andrea Marcus (13), mkazi wa Mbezi-Kibanda cha Mkaa, Dar anadaiwa kuwa wa ajabu kutokana na vitendo vyake. Mtoto huyu amedaiwa kuwa ni wa kichawi kutokana na maajabu yafuatayo: Ana uwezo wa kula ubwabwa sufuria moja la familia, anamudu kunywa maji ndoo moja, ana uwezo wa kuingiza tumboni mikate mikubwa saba kwa mlo mmoja, amewahi kula mchele (si ubwabwa) ndoo nzima. Mbaya zaidi baada ya kula milo hiyo huwa haoneshi ameshiba. Maajabu mengine ambayo yanawashangaza watu wanaoishi naye ni jinsi anavyokula chakula kwa kumwaga chini kisha kukomba mpaka udongo. āSina amani ya moyo, naomba Watanzania wanisaidie, mwanangu ananiuma sana, hata kujisaidia ni hapohapo, chakula anakula kupita kiasi, kama nilivyosema hashibi na bado hali kama mwanadamu wa kawaida,ā alisema mama wa mtoto huyo. Akizungumzia madai ya uchawi,...