Posts

Showing posts from July 29, 2017

Safari ya Kichuya yanukia

Image
Siku chache baada ya kiungo wa Simba, Said Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio katika Klabu ya AFC, mshambuliaji wa timu hiyo, Shiza Kichuya anaweza akapata shavu la kucheza soka nchini Misri. Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema klabu moja ya Misri inamtaka Kichuya ili imsajili kwa ajili ya kuichezea timu yao na sasa wapo katika mazungumzo. Bado mazungumzo ya Simba na klabu hiyo yanaendelea na wakifikia muafaka muda wowote Kichuya ataondoka kwenda nchini humo. “Kuna timu ya Misri kupitia wakala aliyemuona Kichuya kwenye ligi na kufanya mawasiliano na sisi na tayari kuna barua wameleta wakimtaka Kichuya. “Kuna dau ambalo wamelipendekeza ili waweze kumsajili Kichuya lakini sisi hatujakubaliana nalo, hivyo tupo katika mazungumzo ya kuweza kufikia makubaliano lakini tunataka waongeze dau. “Hata hivyo, itabidi tumuachie Kichuya akacheze soka la kulipwa kwani kumzuia mchezaji kwa sasa ni sawa na bure, kwani amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na hatut

IGP SIRRO ALIPONGEZA JESHI LA POLISI MKOA WA SINGIDA

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipiga saluti wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua mapema leo kwenye viwanja vya kambi ya FFU mjini hapa. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa jeshi la polisi mjini Singida leo piga saluti wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada kukagua askari polisi waliokuwa kwenye paredi kwenye viwanja vya kambi ya FFU mjini hapa. …………………………. Picha/Habari na Gasper Andrew. Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amelipongeza jeshi la polisi Mkoani Singida kwa juhudi zake za kupunguza matukio ya uhalifu yakiwemo ya utekeji wa magari kwa kiwango kikumbwa.IGP Siro ametoa pongezi hizo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kweye viwanja vya kambi ya kikosi c

MAGAZETI YA LEO JULY 29,2017

Image

SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAFUTA GHAFI TOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI TANGA KUFANYIKA AGOSTI 5, 2017

Image
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani anawaalika wananchi katika halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 5, 2017 eneo la Chongoleani jijini Tanga ambapo utahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni. UDUGU WETU, FAHARI YETU - BOMBA LETU KWA MAENDELEO YA WATU WETU

Maazimio ya Baraza Kuu la CUF Lililokutana Leo Zanzibar

Image
Baraza kuu la Uongozi la Taifa la CUF ijumaa ya Julai, 28 limekutana kujadili mambo mbalimbali ambayo yanahusu chama hicho ikiwa ni pamoja na kujadili uamuzi wa CUF ya upande wa Prof. Lipumba kuwavua uanachama wabunge nane jambo lililofanya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwavua auanachama. UTANGULIZI: Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) leo hii Ijumaa, tarehe 28 Julai, 2017 limefanya kikao cha dharura kilichoitishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama ya mwaka 1992 (Toleo la 2014), kifungu cha 80 (1). Wajumbe 45 kati ya wajumbe 52 halali wa Baraza Kuu wamehudhuria ambao ni sawa na asilimia 86 ya wajumbe wote. Katika kikao hiki, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu ajenda moja tu iliyowasilishwa kwake na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo ilikuwa ni: • Taarifa kuhusu kile kinachoitwa kuwavua uanachama Wabunge wanane (8) na Madiwani wawili (2)