MBUGA ZA WANYAMA UNAZOWEZA KUTEMBELEA BURE WIKENDI HII
Siku ya Jumatatu ya Juni 5 itakuwa ni maadhimisho ya ‘Siku ya Mazingira Duniani’ ambayo huadhimishwa na mataifa tofauti duniani ikiwa imebeba kauli mbiu ya ‘Kuwaunganisha Watu na Mazingira Asilia.’ Mapema wiki hii Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba alitoa taarifa kwa umma kuwa kwa hapa nchini maadhimisho ya siku hiyo kitaifa yatafanyika kijijini Butiama mkoani Mara, mahali alipozaliwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl. Julius Nyerere, ikiwa ni kuenzi jitihada zake za kulinda na kuhifadhi mazingira. Katika kunogesha sherehe hizo Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa ofa kwa wananchi kutembelea hifadhi yoyote ya mbuga ya wanyama bila ya kiingilio chochote kwa siku tatu, kuanzia Ijumaa ya Juni 2 mpaka Jumapili ya Juni 4. Alisema kuwa lengo kubwa ni kuona uwepo wa wanyama na kujifunza kuwa mazingira yanahitaji kulindwa zaidi na zaidi. Kauli hiyo ya Waziri imekuja si...