Posts

Showing posts from March 23, 2017

MBUNGE HUSSEIN BASHE AMWANDIKIA UJUMBEE HUU NAPE NNAUYE

Image
Leo March 23, 2017 kumefanyika mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Dkt. John Pombe Magufuli   amemteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria   Dkt. Harrison George Mwakyembe   kuongoza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo ilikuwa chini ya   Nape Nnauye . Baada ya mabadiliko hayo watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa wamekuwa wakilizungumzia hilo katika page zao za mitandao ya kijamii miongoni mwao ni Mbunge wa Nzega Mjini  Hussein Bashe   ambaye aliamua kuandika ujumbe kupitia account yake ya Twitter huku akimtaka Nape Nnauye kutovunjika moyo. Bashe ameandika>>> “Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It’s just beginning of a New journey.”   Follow Hussein M Bashe   @HusseinBashe Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It's just beginning of a New journey....

Maneno ya Waziri Nape mchana huu Kuhusu Ripoti ya Tukio la Makonda

Image
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo  Nape Nnauye jana March 20, 2017 alifanya ziara makao makuu ya Clouds Media Group baada kuwepo taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa Kipindi cha SHILAWADU kurusha kipindi chake. Waziri Nape aliunda Tume ya uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo na kutoa saa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Makonda na watu wake kisha leo March 21 iwasilishwe. Baasa ya kuona anapigiwa simu nyingi za kuhoji hatua iliyofikiwa hadi sasa Waziri Nape ametoa majibu kupitia Account yake ya Twitter na kusema ’Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!‘

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WATEULE NCHINI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) leo tarehe 22 Machi, 2017 amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule 7 wanaowakilisha nchi zao nchini kutoka Hungary, Belarus, Guinea, Botswana, Niger, Cyprus na Bangladesh. Pichani Balozi Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Hungary nchini, Mhe. Laszlo Eduard Mathe mwenye makazi yake Nairobi, Kenya.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Belarus nchini, Mhe. Dmitry Kuptel mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Balozi Mteule wa Guinea nchini Mhe. Sidibe Fatoumata KABA mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia mara baada ya kupokea Nakala zak...

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BALAZA LA MAWAZIRI

Image