HAUSIBOI ALIYEMLAWITI BINTI WA MIAKA MINNE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA HUKO MPANDA
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemhukumu kijana, Baraka Juma (22) mkazi wa kijiji cha Nkungwi wilayani humo, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne baada ya kumhadaa na kumlewesha bia. Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alisema ameridhishwa na ushahidi pasipo kutia shaka uliotolewa mahakamani hapo na upande zote mbili za mashitaka na utetezi. “Nimelazimika kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa baada ya mahakama hii kumtia hatiani ili iwe fundisho si kwake tu, lakini pia kwa wengine wenye tabia kama yako .... kitendo ulichomtendea mtoto huyo ni cha kinyama hustahili ...