Posts

Showing posts from August 13, 2018

KIFO CHA MAJUTO… KILICHOMTOA FAHAMU TAUSI CHA JULIKANA

Image
S IRI ya muigizaji Tausi Mdegela, kuangua kilio kupita kiasi kwenye msiba wa nguli wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘King Majuto’ wiki iliyopita imebainika kuwa msanii huyo alikuwa ni baba yake wa hiari aliyemfundisha sanaa ambayo sasa inamweka mjini. Akizungumza na Ijumaa wa Wikienda, Tausi alisema kuwa, Majuto alikuwa baba yake aliyemlea katika maadili mema na aliyetamani sana kumuona anafika mbali kisanaa kwani ndio aliyemfundisha na alikaa naye nyumbani kwake Tanga kwa muda mrefu kama mwanaye wa kumzaa. “Mimi hapa nalia kwa uchungu mkubwa naumia mno kumpoteza baba yangu aliyenilea katika kazi kwa sababu ni mtu ambaye alikuwa anataka kujua hali yangu kila mara na alipenda mno kuona maendeleo yangu kila siku kama mwanaye,” alisema Tausi. Akiendelea kuzungumza na gazeti hili kwa uchungu, Tausi alisema kuwa Mzee Majuto hata wakati anakaribia kufariki yeye alikuwa ametoka nje kidogo ya Jiji la Dar lakini alipigiwa simu na dairekta Leah Mwendamseke ‘Lamata’ na ku...

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO YA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 19. Taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Bi. Senyi Simon Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza. Bi. Senyi Simon Ngaga amechukua nafasi ya Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Chato aliyeteuliwa hivi karibuni Kanali Patrick Norbert Songea kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi nje ya nchi. Uteuzi wa Bi. Senyi Simon Ngaga unaanza leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Wakuu wa Wilaya wote wawili wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao ...

RAIS MAGUFULI APONGEZA JIMBO LA MBULU KUPATA ASKOFU MPYA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria profesa Palamagamba Kabudi na Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na viongozi mbalimbali wakifuatilia misa Takatifu ya kumweka wakfu Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen. Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen akiwekwa wakfu kuwa askofu wa Jimbo hilo mjini Mbulu Mkoani Manyara jana. Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen akiwa kwenye kiti chake baada ya kusimikwa kushika nafasi hiyo mjini Mbulu Mkoani Manyara jana, kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Dar es salaam mhadhama Polycap Kardinali Pengo na Askofu mwandamizi Yuda Thadeus Ruwaichi. Waziri wa Katiba na Sheria profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu Anthony Lagwen, zawadi iliyotolewa na Rais John Pombe Joseph Magufuli baada ya Askofu huyo kusimikwa jana mjini Mbulu Mkoani Manyara. RAIS John Magufuli amewapongeza wananchi wa wilaya za Mbulu, Babati na Hanang’ mkoani Manyara na Karatu mkoani Arusha zin...