Linah asema hufanya kusudi kuwapagawisha vidume awapo jukwaani
Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga maarufu kama 'Ndege Mnana' amefunguka na kuweka wazi kuwa huwa anafanya makusudi kuvaa nguo za nusu utupu 'fupi' akiwa kwenye show ili aweze kuwapagawisha watoto wa kiume walioko katika tamasha ambalo anashiriki. Linah amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa kijamii facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati. "Mashabiki zangu wengi ni watoto wa kiume hivyo wakiona vichuchu vimesimama wanapata raha sana, muda mwingine nawatega kwa mavazi kwenye 'show' ili waburudike hivyo siwezi kubadili mavazi yangu kwa sababu mimi ni msanii ila ikitokea natakiwa kwenda sehemu ya kuvaa mavazi marefu ntafanya sina jinsi", amesema Linah. Kwa upande mwingine, Ndege Mnana amesema wakati mwingine huwa anapata wakati mgumu kutokana na mavazi yake akiwa jukwaani kwani akimuuita ...