Star wa "Prison Break" Wentworth Miller a.k.a Michael Scofield amejiweka wazi kuwa yeye ni Shoga
Star wa "Prison Break", Wentworth Miller a.k.a Michael Scofield, amejitangaza kuwa yeye ni "Gay" (shoga), katika barua ya wazi aliyoiandika kwenda kwa Directoe wa St. Petersburg International Film Festival (tamasha la filamu la kimataifa la St. Petersburg). Muigizaji huyo (41) ameandika barua hiyo kukataa mualiko uliokuwa ukimtaka kuhudhuria tamasha hilo linalofanyika nchini kwao Russia na kwa mara ya kwanza kupitia barua hiyo amejitangaza kuwa yeye ni "Gay" (shoga). "Asante kwa ukarimu wa mualiko wako, nikiwa kama mtu ambaye amefurahia kutembelea Russia kwa miaka ya nyuma na naweza pia kudai shahada ya asili ya kirusi, ningefurahi kusema ndio, hata hivyo nikiwa kama shoga (gay) lazima nikatae". amesema Miller Miller akaendelea kusema ... nasumbuliwa sana na tabia ya sasa dhidi ya na jinsi wanavyochukuliwa mashoga na wanawake na serikali ya Urusi. "hali hii haikubaliki kabisa kwa namna yoyote ile , na ...