Wema atumbua Mil.300
Wema Sepetu ‘Madam’. Na Mwandishi Wetu WEMA Sepetu ‘Madam’ ni mashine ya kutafuna fedha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari za mjini kumtaja staa huyo wa Bongo Movies kuwa ameteketeza takriban Sh. Mil. 300 za mbunge ambaye anadaiwa kuwa ndiye anayemweka mjini kwa sasa, Risasi Mchanganyiko limenasa ubuyu kamili. KUMBUKUMBU MUHIMU Wema na mbunge huyo (jina kapuni kwa sasa) wanadaiwa kuwa walianzisha uhusiano wa kimapenzi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana ambao matokeo yake yalimpa ushindi Dk. John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Inadaiwa uhusiano huo tayari umezaa matunda kwani mlimbwende huyo ni mjamzito. TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya mrembo huyo asiyechuja Bongo kuwa ‘klozi’ na mbunge huyo kijana mwenye pesa ndefu katika kampeni hadi sasa, amemchuna mbunge huyo kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matumizi na zawadi mbalimbali ali...