Posts

Showing posts from December 25, 2016

WAKRISTO WALIVYOSHIRIKI IBADA YA MKESHA WA KRISMASI JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akisalimiana na muumini wa kanisa hilo Usahrika wa Azania Front, Violet Muro baada ya kumpatia zawadi ya ibada mkesha wa Krismasi iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam. Kwaya ya Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Akbano ikitumbuiza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam. Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa krismasi.  Vijana wa Kanisa la KKKT la Azania Front wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo.  Kwaya ya Vijana ya KKKT usharika wa Azania Front ikitoa burudani.  Kwaya ya vijana ya KKKT Usharika wa Azania Front ikiendelea kutoa burudani.  Watoto wakishiriki ibada katika Kanisa la KKKT la Azania Front  Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akimsalimia muumini wa kanisa hilo, Violet Njau aliyekuwa ameongoza na...

MAMBO Yanayoshusha Thamani ya Mwanaume Mbele ya Mwanamke

Image
Katika uhusiano baina ya mume na mke hutokea mambo mbalimbali yanayoimarisha uhusiano baina yao au kuuharibu. Baadhi ya nyakati mwanaume hufanya baadhi ya mambo yanayomshusha thamani mbele ya mwanamke. Hivyo, wanaume wote wenye khofu ya heshima na thamani yao kuanguka, ninawaletea mambo muhimu ambayo yanashusha thamani ya mwanaume mbele ye mwanamke: 1. HADAA NA UNYONYAJI: Baadhi ya wanaume ni wazuri sana katika kumnyonya mwanamke kwa kutumia kisingizio cha mapenzi. Wanazitumia mali zake na kuzinyonya kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na maneno matamu ya mapenzi au kutengeneza simulizi za uongo kuhusu matatizo ya kipesa na kiuchumi. Mwanamke akigundua kuwa analaghaiwa, basi atamshusha thamani haraka mwanaume huyo na kuamua kujitenga naye. Na iwapo ataendelea kuwa naye, basi hasara na majuto yatakuwa juu ya mwanamke huyo. 2. WANAWAKE WENGI: Mwanamke anapenda ahisi kuwa yeye ndiye mtu pekee katika maisha ya mwanaume. Kuwa na uhusiano na wanawake wengi...

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 25.12.2016

Image

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI SINGIDA, ANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KRISMASI

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuwasili mkoani humo. Pia Rais Dkt. Magufuli anatarajiwa kushiriki katika Ibada ya Krismasi mkoani humo hapo Kesho  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akielezea ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki katika Ibada ya Siku ya Krismasi katika Kanisa mojawapo mkoani Singida. PICHA NA IKULU