Posts

Showing posts from June 14, 2016

Pichaz 15: CRDB wamemkabidhi Paul Makonda milioni 100

Image
  Baada ya Rais Magufuli kutangaza elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka kufikia kidato cha nne, kumekuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa madawati ambapo Serikali ilianzisha kampeni ya uchangiaji wa madawati, leo June 14 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam   Paul Makonda  amepokea milioni 100 kutoka Bank ya CRDB kwa ajili ya manunuzi ya madawati katika Mkoa wa Dar es Salaam , ‘ Nimeshaongea na wakuu wangu wote wa Wilaya popote pale ambapo upo waje na mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nitapokea chochote kile hata kama liwe ni dawati moja nitalipokea ‘ >>> Paul Makonda

Aina mbalimbali ya maumivu ya tumbo

Image
Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo. Maumivu chini ya mbavu: Kulia yanaweza kusababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo, maambukizi kwenye mfuko wa nyongo Cholecystitis , uvimbe wa ini, jipu kwenye ini, saratani ya kongosho na kifuko cha nyongo. Maumivu chini ya chembe ya moyo: Husababishwa na vidonda vya tumbo, kiungulia, saratani ya tumbo na saratani ya kongosho. Maumivu pembeni mwa kitovu: husababishwa na mawe ya figo Kidney Stones, maambukizi ya figo, Pyelonephritis na  maambukizi kidoletumbo Acute Appendicitis Maumivu chini ya kitovu: huweza kusababishwa na maambukizi ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya zinaa kama klamidia, PID, vivimbe vya mji wa uzazi, mimba kuharibika na saratani ya kibofu cha mkojo. Maumivu ya tumbo: Ni utumbo kujiziba Intestinal Obstruction,  utumbo kujisokota Volvulus, kula sumu na  mzio wa chakula fulani au ugonjwa wa Crohn Crohn’s Disease,  Ngiri He...

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AGAWA FUTARI KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NA KUJIONEA MABASI YA MWENDO KASI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteremka kwenye basi la mwendo kasi baada ya kupanda na kujionea ubora na uzuri wa mabasi hayo ambayo yamerahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.( Picna na OMR) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalumu wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongoza dua hiyo Mussa Salum . Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Futari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwale wakati wa shu...

Umuhimu wa maziwa mwilini

Image
Unywaji wa maziwa unaopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)  ni mtu mmoja kunywa lita 200 kwa mwaka. Tovuti za Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) zinaonesha kuwa Mtanzania hunywa wastani wa lita 47 tu kwa mwaka. Wakati unywaji huo wa maziwa si wa kuridhisha, kiwango cha watoto wetu kudumaa bado ni kikubwa ambapo asilimia 35 hudumaa. Sababu kubwa inayofanya watoto hao kudumaa ni ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho mwilini. Maziwa yana virutubisho vyote muhimu kwa ujenzi wa afya ya binadamu kwani yana protini ya daraja la kwanza, mafuta, madini, vitamin na sukari ya asili ya lactose na maji. Maziwa hutupatia takriban vitamini zote ambazo huyeyuka kwenye mafuta. Nazo ni vitamini A, D, E na K. Vitamini A huhusika na shughuli mbalimbali mwilini. Mfano afya bora ya ngozi zetu kuwa nyororo na ng’avu na pia kuwa na uwezo wa kuzuia wadudu wasiingie mwilini. Vile vile vitamini A hutumika pia kuyapatia macho uimara wa kuona. Na hasa kuona usiku au kwenye mwanga hafifu. Ukosefu wake...

PROFESA LIPUMBA AOMBA MADARAKA TENA…. ..AANDIKA BARUA YA KUOMBA KUENDELEA UENYEKITI WA CUF.

Image
Mwenyekiti wa zamani wa CUF,Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa amemwandikia Katibu Mkuu wa chama hicho barua ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu Uenyekiti wa CUF. Sasa anasubiri majibu toka kwa Katibu Mkuu,Maalim Seif,baada ya ombi lake kujadiliwa na ngazi za juu za kichama. Pia amesema Bajeti ya mwaka wa Fedha 2016/17 yenye thamani ya zaidi ya Trilioni 29.5 haiendani na uhalisia.