Posts

Showing posts from December 12, 2015

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukum

BREAKING NEWZZZZ!! KILICHOJIRI MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA LEO,JAMES LEMBELI APENYA KIZINGITI CHA KWANZA

Image
Kushoto ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli (Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo asubuhi baada ya kushinda maombi yao ya kuomba kupunguziwa gharama za kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi uliompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Jumanne Kishimba ambapo Lembeli alipaswa kulipa shilingi milioni 15 na badala yake Mahakama imemtaka kulipa Shilingi milioni 9 ndipo kesi ya msingi ianze kusikilizwa-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog Lembeli akitoka Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga akiwa na uso wa furaha baada kuvuka kiunzi cha kwanza katika kesi namba 1 ya mwaka 2015 aliyofungua Novemba 23,mwaka huu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM,Jumanne Kishimba,katika uchaguzi mkuu uliopita nchini Tanzania Baada ya kufungua kesi hiyo James Lembeli

WATUHUMIWA 40 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UKWEPAJI KODI.

Image
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu. Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi w