Posts

Showing posts from December 23, 2014

ALICHO POST ZITTO KABWE, BAADA YA RAIS KUMVUA MADARAKA WAZIRI ANNA TIBAIJUKA

Image
Nimemsikiliza Mhe Rais. Ninachoweza kusema ni kwamba maazimio yale hayakuwa ya  Zitto Kabwe , PAC, CAG au PCCB. Yalikuwa ni maamuzi ya Bunge zima. Bunge la vyama vyote kikiwamo chama cha Rais Kikwete yaani CCM. Sisi kama Bunge tulitoa maazimio yale kwa maridhiano, uzalendo na bila kutaka kumuonea mtu yeyote. Suala hili sasa naliacha kwa wananchi. Bunge limefanya kazi yake na Serikali ambayo ndiyo tulikuwa tunasubiri maamuzi yake imeamua hivyo. Wananchi wataamua wenyewe. NAWEWE TOA MAONI YAKO HAPA CHINI USIKIKE !

HAYA NDIYO MADHARA YA KUKU WA KISASA

Image
Kwa muda mrefu watu wengi amekuwa wakiwafakamia kuku hawa pasipo kujua madhara yao.  Je umewahi kujiuliza na kutafakari madhara ya ndege hawa watamu??? Yatambue madhara yake hapa.  Kuku hawa tofauti na kuku wa kienyeji hukua kwa haraka sana kutokana na vyakula vya kemikali nyingi walishwazo.ndani ya miezi miwili kuku hawa huwa tayari kwa kitoweo tangu watotolewapo.tena hutotolewa kwa mashine.  wakati kuku wa kienyenj huchukua hadi miezi nane kuwa tayari kwa kitoweo,na hutotolewa na mama zao. MADHARA YAKE NI HAYA.   1.Kwa watoto kukua kwa haraka na kupevuka kimaumbile mapema mno.  2.Kwa Wakubwa;wanaume kunenepa sana na kuota matiti kama wanawake. 3.Kwa wanawake;kuota ndevu kama wanaume,kuwa na vipara kicchwani,na miili legelege kwa wote.  JE,WAJUA NA NINI MAONI YAKO?

WOLPER ADAI HAKUWAHI KUVAA NGUO FUPI .....LAKINI HII YA LEO NI BAHATI MBAYA TU

Image
Mrembo na mwigizaji wa kike wa filamu hapa nchini, Jackline Masawe “Wolper” amekuwa akisifiwa kwa kuvaa nguo za heshima ukilinganisha na mavazi wanayovaa baadhi ya mastaa wengine hapa Bongo wakiwa mitaani au kwenye burudani Sasa jana mrembo huyu akatupia picha hizi akiwa beach amevalia ka-pensi keupe huku juu amavalia brauzi nyeusi na kofia nyeupe kichwanina huku akicheza na ka-"DOG" ..Kisha akawaandikia hivi mashabiki wake; "Sikuwahi kuvaa nguo fupi wakati naenda kanisani au sokoni nawakati wote mmekua mkinisifia navaa nguo za heshima sasa mkitaka niiheshm paka beach mtakua mmetishaa saana wana ndugu mnaojua sheria humu insta so mnataka beach nivae kanic au komeni pita like utaki pita". Mdau umeionaje hii!!!!

NI VITA KARIAKOO,RISASI ZA ZARINDIMA NJENJE,MAGARI SOMA HAPA KUJUA

Image
Vurugu kubwa imetokea mda huu maeneo ya kariakoo Jijini Dar Es Salaam na kupelekea Jeshi la polisi kurusha Risasi hovyo ili kuwatawanya Wamachinga walioanzisha Fujo hizo huku barabara za kuingia na kutoka kariakoo zikiwa zimefungwa kutokana na Matairi ya Gari yaliyochomwa moto barabarani.  Kwa Mujibu wa Shudhuda wetu aliyoko Maeneo hayo ya Kaliakoo anasema Chanzo cha vurugu hizo zinatokana na Wafanyabiashara Wadogodogo Maarufu Wamachinga kudai mfanya Biashara mwenzao kuuliwa na Mgambo wa jiji. Shuhuda huyo alizidi kusema Mfanya Biashara huyo aliuliwa na Mgambo kwa kupigwa kipigo kikali na kumpelekea mauti, Wafanyabiashara hao wanadai hali hiyo ni ishara ya kuchoshwa na Manyanyaso hayo wanayofanyiwa na Mgambo hao na kuanzisha hali hiyo ya Fujo ambayo wanadai ni njia ya kupeleka ujumbe kwa Serikali

OKWI HATI HATI KUIVAA KAGERA SUGAR FC IJUMAA

Image
Mshambuliaji anayetajwa kuwa ‘mtukutu’ wa Simba, Mganda Emanuel Okwi yuko hatarini kuikosa mechi yao inayofuata dhidi ya Kagera Sugar FC. Simba SC iliyoweka kambi Visiwani Zanhzibar tangu jana mchana, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Kagera Sugar FC katika mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Ijumaa. Mratibu wa kambi ya Simba SC visiwani humo, Abdul Mshangama ameuambia mtandao huu kuwa Okwi anatarajiwa kujiunga na timu yao Alhamisi akitokea kwao Uganda alikoenda kwa ajili ya kufunga ndoa. Okwi alifunga ndoa juzi na amekuwa na desturi ya kutorejea katika klabu anazosajiliwa wakati wa sherehe za Krismas ambayo ni siku yake ya kuzaliwa mwaka 1992. “Okwi anatarajia kuja kuungana nasi Alhamisi,” amesema Mshangama. Kama Okwi atarejea nchini siku hiyo ya Sikukuu, nbi wazi kwamba hatakuwa na nafasi ya kukipiga katika kikosi cha kocha Mzambia Patrick Phiri cha Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MSANII NASEEB ABDUL ‘DIAMOND’ IKULU, AWAPONGEZA YEYE NA IDRIS SULTAN KWA KUILETEA SIFA TANZANIA DESEMBA 23, 201

Image
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha msanii Naseeb Abdul “Diamond”  na  kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya  tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Profesa Hermas Mwansoko. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond”  juu ya ushindi wake wa  tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na msanii Naseeb Abdul “Diamond”  alipomkaribisha Ikulu   kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jiji

KATIBU MKUU KIONGOZI AMSIMAMISHA KAZI KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHARTI NA MADINI

Image
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.” Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara y