Rais Magufuli: Tumejipanga Kununua Ndege Mpya Kubwa Mbili
Ndege mbili aina ya Bomberdia zilizozinduliwa jijini Dar es Salaam leo. Vikundi vya ngoma vikitumbuiza katika uzinduzi wa ndege mbili aina ya Bomberdia jijini Dar es Salaam leo RAIS John Magufuli amesema serikali yake imejipanga kununua ndege nyingine mbili ambapo moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine abiria 242. Hayo ameyasema leo wakati akizindua ndege mbili za serikali kwenye hafla iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere uliopo jijini Dar es Saalam. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mama Janeth Magufuli; Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbawara; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam Paul Makonda; Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Saalam Isaya Mwita na viongozi wengine mbalimbali. Vilevile rais aliwananga watu wote wanaobeza ununuzi wa ndege hizo na kuziita zina kasi ndogo ya Bajaj akawataka wawe na moyo wa kupenda vitu vyao wenyewe. Pia amewahakikishia Watanzania kwa ujumla kwamba nde...