KAJALA ANAPATA WAPI JEURI HII?
Imelda mtema FEDHA inaongea! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mwigizaji Kajala Masanja kupanga kwenye mjengo mpya wa maana na kuushehenesha samani na ‘vikorombwezo’ kibao hadi kufikia hatua ya watu kuhoji, amepata wapi jeuri hiyo ya fedha? Ijumaa limenasa mchapo kamili. Mjengo anaoishi mwigizaji Kajala Masanja. Kajala ambaye awali alikuwa akiishi maeneo ya Sinza-Madukani, kwa sasa amehamia katika mjengo huo mpya uliopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo, ndani ya mjengo huo, Kajala anaishi na mwanaye Paula huku akiwa amewaajiri wafanyakazi wa ndani watatu na kulindwa na kampuni maalum ya ulinzi. “Yani Kajala ananuka hela. Mjengo wake mpya una kila kitu ndani. Ukiingia unaweza kupagawa kutokana na vitu vilivyomo ndani. Watu tunajiuliza ni nani anayempa jeuri hii maana filamu pekee haziwezi kufanya matusi haya,” kilisema chanzo hicho. ...Sebuleni. Baada ya kupenyezewa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alitia timu nyumbani hapo kwa Kajala na ...