Ngoma, Bossou kuikosa Prisons
MSHAMBULIAJI Donald Ngoma na Vincent Bossou watakosekana katika kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kuivaa Tanzania Prisons kutoka Mbeya katika mechi ya hatua ya ya robo ya fainali ya mashindano ya Kombe la FA itakayofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wataingia uwanjani huku wakiwaheshimu wapinzani wao kutokana na uzoefu waliokuwa nao kwenye ligi na mashindano mbalimbali. Mwambusi alisema kuwa wamejiandaa na ushindani na changamoto kutoka kwa Prisons ambayo wachezaji wake wamekaa pamoja muda mrefu. 'Hatutawadharau Prisons, mpira hauna historia, tusubiri tuone dakika 90, ila tutamkosa Vincent ambaye ni mgonjwa aliumia jana (juzi) na leo (jana) amekwenda hospitali, Ngoma ndio hatokuwapo kabisa, aliumia tangu tulipokuwa safarii, tunasema mchezo wa kesho utakuwa mgumu zaidi, " alisema Mwambusi. Aliongeza kuw...