Zuckerberg Akiri Kosa Lake Na Kuomba Radhi
Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg. Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg ametoa maelezo katika Bunge la Marekani- Congress kwa mara ya kwanza Jumanne, akijibu wasiwasi ulioelezwa na wabunge juu ya kushindwa kwa mtandao wa jamii maarufu kulinda taarifa zao. Taarifa hizo za siri ni za watumiaji wanaofikia milioni 87 ulimwenguni zilizotumiwa na kampuni yenye kujishughulisha na siasa- Cambridge Analytica iliyokuwa na mafungamano na Trump. Mahojiano hayo yanaendelea Jumatano wakati Zuckerberg atakapokutana katika raundi ya pili kujibu maswali mbele ya jopo la Wabunge wa Marekani. Mkurugenzi huyo Mark Zuckerberg amekiri kuwa :”Hilo lilikuwa kosa kubwa na ni kosa langu mimi mwenyewe na naomba radhi. Nilianzisha matandao wa Facebook, niliusimamia na nina wajibika kwa kitu chochote kinachotokea.” Wachambuzi wanasema ni kosa ambalo liliruhusu kampuni ya kisiasa ya Cambridge Analytica kupata taarifa kwa kupitia programu iliyotengenezwa na k...