SOLLY MAHLANGU ‘OBRIGADO’ KUOMBELEZA KIFO CHA MANDELA UWANJA WA TAIFA
Na Makuburi Ally WAKATI siku za Tamasha la Krismasi zikikaribia, Muimbaji mahiri anayeshika kasi katika anga la muziki wa Injili barani Afrika, Solly Mahlangu anatarajia kuombeleza kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela anayetarajia kuzikwa keshokutwa kijijini Qunu nchini humo. Baadhi ya waumini watajiuliza maswali mengi kwamba baada ya kifo cha Mandela labda muimbaji huyo hatoweza kushiriki katika Tamasha hilo la kumtukuza na kumuimbia Mungu, lakini ukweli ni kwamba wamtarajie muimbaji huyo ambaye ataimba baadhi ya nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha hilo, Alex Msama, muimbaji huyo ni mmoja wa waimbaji kutoka nje ya Tanzania ambao watashiriki, hivyo waumini watarajie kumuona jukwaani akifikisha neno la Mungu kwa njia ya nyimbo. “Ni muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa injili bar...