JE WAJUA MUME ANAWEZA KUMFANYA MKEWE KUWA ZUZU?!!!...
Ni wazi unawajua wanawake ambao wanaishi katika ndoa ngumu za manyanyaso hadi unafikia kuuliza, ‘hivi huyo mwanaume amempa kitu gani kikubwa hivyo?’ Wanawake hawa nao wanakuwa wamefikia mahali ambapo wanaamini kuwa wanatakiwa kuishi hivyo, kwenye uhusiano wa ain hiyo. Ni kitu gani kinatokea hadi mwanamke kuamini kwamba yeye ameandikiwa kuishi kwenye ndoa ya shida na karaha na mwingine kuamini kwamba hivyo ndivyo ndoa zinavyotakiwa kuwa? Malezi na mazingira ni moja ya sababu kuu, lakini usugu ni sababu nyingine. Ninaposema usugu nina maana kwamba mwanaume anatokea kumdhalilisha mwanamke na mwanamke huyo kuvumilia hadi anajikuta amefikia kuamini kwamba hiyo ndio ndoa, hivyo ndivyo anavyostahili kuishi. Mwanmke anapovumilia mateso ya ndoa kwa muda mrefu sana bila kujua ni kwa nini au kwa matarajio kwamba mmewe atabadilika, hufikia mahali ambapo kujiamini kwa mwanamke huyo huisha na hujishusha kithamani na kuwa chini kabisa. Hebu jaribu kuwachunguza wa...