Posts

Showing posts from July 1, 2013

MMILIKI WA FACEBOOK NA WAFANYAKAZI WAKE WASHEREHEKEA KUPITISHWA KWA SHERIA YA NDOA YA JINSIA MOJA

Image
Mmiliki wa mtandao wa kijamii Facebook CEO Mark Zuckerberg amejiunga na wafanyakazi wa kampuni yake waliozidi 700 katika matembezi ya kusherekea maamuzi ya mahakama kuhusu haki za ndoa ya jinsia moja. Matembezi haya yamefanyika mitaa ya San Francisco Jumapili Asubuh. Sheria hio inayo sherekewa Imeruhusu wanandoa wa jinsia moja kumiliki leseni ya ndoa ndani ya siku 30 baada ya kuoana. 

HUU NDO MWONEKANO MPYA WA AGNESS MASOGANGE,HAKIKA AMETOKELEZEA MBAYAA

Image
Baadhi ya Picha chache Mpya za Agness Masogange ....Hizi amezitupia kwenye Instragram yake .

MAKAMU WA RAIS KENYA ADAI KENYA INA MARAFIKI WENGI TOFAUTI NA MAREKANI NA KAMWE HAWAWEZI KURUHUSU SERA YA USHOGA YA OBAMA

Image
NAIBU wa Rais Bw William Ruto, jana alivunja kimya chake kuhusu hatua ya rais wa Marekani Barack Obama kutozuru humu nchini kwa kusema hatua hiyo haina madhara yoyote kwa Kenya. Huku akiongea katika kanisa la Katoliki la St Gabriel Bahati, kaunti ya Nakuru,  Bw Ruto alisema nchi hii ina 'marafiki’ wengine wengi duniani ambao inaweza kushirikiana nao huku akiongezea kuwa hatua ya rais Obama kukwepa kutembelea Kenya haiwezi kutatiza kwa vyovyote vile uhusiano mwema uliopo wa kibiashara baina ya Marekani na Kenya. “Tunaiheshimu nchi ya Marekani nayo inafaa kuwaheshimu Wakenya,” akasema Bw Ruto. Alisema serikali tayari imeanzisha mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na mataifa  mengine  huku akikariri kuwa  safari ya Rais Uhuru Kenyatta nchini Uganda ambapo alikutana na rais wa nchi hiyo Yoweri  Museveni na mwenzao wa Rwanda rais Paul Kagame kujadili jinsi nchi hizo tatu zinaweza kushirikiana kibiashara, ni miongoni mwa mi

MATUKIO YA RAIS BARACK OBAMA AKIWASILI NCHINI MCHANA HUU, TAZAMA PICHA ZA KILA KILICHOJIRI AIRPORT

Image
Rais Barack Obama wa Nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba na watoto wao, wakiwasili mchana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku mbili hapa nchini. Ndege ya Raisi wa Marekani Ikiwa Kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mgeni wake wa Marekani, Barack Obama aliewasili nchini Mchana huu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Rais Barack Obama akikagua Gwaride maalum aliloandaliwa akiongozwa na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenelari Davies Mwamunyange. Rais barack Obama akiagana na mama Salma Kikwete Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere. Msafara wa Viaongozi ukiondoka Uwanja wa Ndege. Picha zote kwa Hisani ya TBC1 TOA MAONI YAKO HAPA CHIN

PICHA ZA RAIS OBAMA ALIPOTUA KATIKA ARDHI YA TANZANIA

Image
 Rais Baraka Obama akicheza ngoma alipokua akipita kwenye moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbuiza kwa ajli ya ujio wake mara tu aliposhuka kutoka kwenye ndege ya Airforce One  Mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete akitabasamu wakati mgeni wake Rais Barack Obama alipokua akitikisa mwili kwa hisia za ngoma za asili zilizokua zikitumbuizwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa ujio wake leo akitokea Afrika ya Kusini.  Rais Barack Obama akiangalia moja ya vikundi vya ngoma za asili vilivyokua vikitumbuiza uwanjani hapo.  Rais Barack Obama akikagua majeshi ya ulinzi na usalama. Rais wa Marekani Barack Obama pamoja mkwewe wakilakiwa na mwenyeji wao Rais Jakaya Kikwete mara tu walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere leo Jumatatu July 1, 2013 kwa ziara ya siku 2., kushoto ni mama Salma Kikwete.   Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama akipokewa kwa Shangwe Ikulu, Dar es

WAGHANA WAMLAANI NANDO WA TANZANIA KWA KUZINI NA DEMU WAO ( SELLY) NDANI YA BBA......MAMA MZAZI WA BINTI AMTETEA

Image
  Wiki iliyopita wapenzi Nando wa Tanzania na Selly wa Ghana  waliucheza ule mchezo wa kikubwa   katika Big Brother ‘The Chase’ inayoendelea, na inasemekana baada ya Ghana na Afrika kwa ujumla kushuhudia mechi hiyo ya kirafiki watu wa karibu na mpenzi wa Selly wamemshauri ampige kibuti. Wote tunafahamu kwamba washiriki wote wa BBA wana maisha yao nje ya Big Brother na inawezekana kila mmoja anamahusiano huko alikotoka, lakini mission iliyowapeleka BBA ‘The Chase’ ni kushinda $300,000 inayomsubiri kinara mmoja, na ili kupenya njia nyembamba za kuufikia ushindi kila mmoja anajitahidi kufumba macho na kujisahaulisha kama camera ziko on ili aweze ku accomplish mission hiyo bila kujali njia anazotumia. Baada ya video clip ya wapenzi wa BBA The chase Nando na Selly wakifanya mapenzi kusambaa ,baadhi ya watu wa karibu na boyfriend wa Selly wa Ghana wametoa maoni yao juu ya kitendo hicho cha ‘aibu’. Steven Fiawoo maarufu nchini Ghana kama Praye Ti

GEORGE BUSH NA MKEWE KUTUA NCHINI KESHO

Image
RAIS mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura wanatarajiwa kesho kuwa nchini kuhutubia kongamano linalojadili wajibu wa wake wa marais katika kuinua wanawake duniani. Kuwasili kwa Bush, ni mwendelezo wa wiki hii Jiji la Dar es Salaam kuwa katika pilikapilika za kupokea ugeni wa watu maarufu. Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya George Bush na litafanyika kesho na keshokutwa. Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari , inasema kongamano hilo litahudhuriwa na wake mbalimbali wa marais akiwemo mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama. Pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair atahudhuria. Wake wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji), Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia. Kongamano hilo litajikita zaidi kati

MAANDALIZI YA KUMPOKEA OBAMA YAKAMILIKA...HIZI NI TASWIRA ZA IKULU LEO ASUBUHI

Image
Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda vizuri, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.  Bendera zikiwa zimepangwa na kupangika katika upande wa lango kuu la Mashariki,Ikulu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama. Jengo la Ikulu. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akisoma ratiba. makundi ya wananchi wa Dar es salaam walikishangilia wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipopita kuwasalimia.

HELCOPTA ATAKAYOITUMIA OBAMA ATAKAPOKUJA LEO TANZANIA

Image
Hii ni helcopter ya Obama,inafahamika kama MARINE ONE Hii ni moja ya helcopter za kijeshi zinazokuwa nyuma  ya MARINE ONE alimo Obama MARINE ONE(iliyojitenga karibu na miti)ikiwa imezungukwa  na baadhi ya helcopter za kijeshi,hapo zikiwa zimetuwa mjini Pretoria Africa kusini MARINE ONE ikiwa angani nchini Africa kusin

BRAZIL MABINGWA KOMBE LA MABARA, WAITANDIKA SPAIN 3-0

Image
Hawa ndo wachawi wa soka wakifanya yao pale walipouthirishia ulimwengu kuwa wa ndo mabingwa mara tatu mfululizo Ndiyo maana soka ni mchezo unaopendwa na watu wengi zaidi duniani kwa kuwa hauna matokeo yanayotabirika na Hispania wanaweza kuwa shahidi wa hilo katika mechi ya fainali ya Kombe la Mabara iliyomalizika punde. hapa ni gori la kwanza la ufundi likipachikwa na fred Wenyeji Brazil wametawazwa kuwa mabingwa baada ya kuwafunga mabingwa wa dunia, Hispania kwa mabao 3-0. Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Maraccana ilikuwa burudani tupu na Brazil walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 2 mfungaji akiwa Fred na dakika 44, Neymar akafunga bao la pili kwa shuti kali. Kipindi cha pili, dakika ya tatu, Fred tena akafunga bao la tatu ambalo lilionyesha kumaliza matumaini ya Hispania ambayo baadaye Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penalti. Baada ya hapo, wenyeji ambao walianza soka kwa kasi tokea kipindi cha kwanza, walionekana kuendelea kuwabana mabingw