Posts

Showing posts from April 7, 2016

Mastaa Wajitokeza Kumuenzi Steven Kanumba

Image
Mama mzazi wa aliyekuwa Staa wa Bongo Movie, Marehemu Steven Charles Kanumba, Flora Mtegoa akiwa ameshika shada wakati wa ibada fupi ya kumuombea mwanaye. …Akiweka shada kwenye kaburi la mwanaye,Marehemu Steven Kanumba. Mama wa Staa wa Bongo Movie, Elizabeth Michael, Lucresia Karugila akiweka shada kaburini. Ndugu, jamaa na marafiki wakishiriki kuwasha mishumaa kaburini hapo. Zoezi likiendelea la kuwasha mishumaa kaburini hapo. Taswira ya kaburi lenyewe. Ndugu, jamaa na marafiki wakishiriki ibada fupi ya kumuombea Marehemu, Kanumba kama kumbukumbu ya kutimiza miaka minne toka kifo chake Staa waBongo muvies hapa nchini, Anty Ezekiel akifanya mahojiano na baadhi ya wanahabari makaburini hapo . Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumzia namna Marehemu Steven Kanumba atakavyoendelea kuenziwa tarehe kama ya leo na mwezi, tangu kifo chake. NA DENIS MTIMA/GPL

Hiki ndicho alichokiandika Lulu miaka 4 ya kifo cha Kanumba

Image
app-facebook Lulu Elizabeth Michael 11 hours ago TAREHE NA MWEZI KAMA HUU NDIPO ULITUACHA KIPENZI CHETU, MFALME WA BONGO MOVIE TANZANIA. INATIA SANA SIMANZI KUENDELEZA TASNIA BILA WEWE, MTU WA KWANZA KUUMIA NI MIMI NA MASHABIKI WAKO... MOLA AKUPUMZISHE MAHALA PEMA PEPONI, AMEN! Tafadhali Tumuombee rehma za Mwenyezi Mungu ziwe kwake. Kwa kuonesha upendo kwake share picha hii kwa wengne nao wamuombee.

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 22 YA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishuhudia wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame pamoja na binti yao wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjini Kigali, Rwanda, leo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994 ambapo watu takribani milioni 1,000,000 waliuawa.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiweka shada la maua wakishuhudiwa na wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwan...

Mkuu wa Mkoa wa Arusha apiga marufuku uuzwaji kinywaji cha KIROBA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo.Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata ya Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha. Ntibenda alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa 154, maofisa watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa. Alisema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na wapiga debe. Alisema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa. “Sitaki kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa ...

PICHA ZAIDI ZIARA YA RAIS MAGUFULI NCHINI RWANDA

Image
Taswira Mbalimbali Za Rais Magufuli Na Rais Kagame Wakiwa Nchini Rwanda

Polisi Dar wamchunguza Zari!

Image
Zarina Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah. DAR ES SALAAM: Kufuatia kamatakamata ya wafanya-biashara wanaodaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ‘unga’ Bongo, kuna madai kwamba, Jeshi la Polisi Tanzania linawachunguza upya mastaa wanaoingia na kutoka kwa kutumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar huku Zarina Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah akitajwa kuwemo. Kwa mujibu wa chanzo chetu, hatua hiyo imekuja baada ya jeshi hilo kubaini ‘ingia toka’ ya mastaa hao ambao baadhi yao wamemaliza vitabu vitatu vya hati za kusafiria kwa mwaka mmoja kwa kupigwa muhuri wa uhamiaji kwa sababu ya safari. CHANZO NI HIKI “Mimi nawapa habari, jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania linamchunguza Zari na mastaa wengine wanne, leo siwataji. Kisa ni safari zao za kuingia Tanzania mara kwa mara. “Polisi wanajua kwamba Zari anakuja Bongo kwa sababu ya kumfuata Diamond (Nasibu Abdul) ambaye ni mzazi mwenzake. Ndiyo maana ...

Miaka 4 ya kifo cha Kanumba, hii ndiyo hali halisi.

Image
  Staa wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba enzi za uhai wake. Hii ndiyo hali halisi! Ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba ambapo ametimiza miaka minne kaburini, mambo mbalimbali yametokea tangu alipofariki dunia huku magari na kampuni aliyokuwa akimiliki vikiwa vimepukutika kama majani. Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 maeneo ya Vatcan-Sinza jijini Dar nyumbani kwake alikokuwa akiishi ambapo aliyekuwa mpenzi wake kwa siri, staa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alishikiliwa na polisi na kusweka katika Gereza la Segerea kwa mwaka mmoja, akidaiwa kuhusika na kifo chake kwani ndiye aliyekuwa naye chumbani usiku huo. TASNIA YA FILAMU Tangu Kanumba aondoke, tasnia ya filamu imedorora na wasanii wengi wamekuwa wakikiri kwamba ni kutokana na kifo cha staa huyo kwani ndiye aliyekuwa chachu na changamoto kubwa ambayo ilikuwa ikisababisha wengine kufanya kazi kwa bidii ili wamfikie au pengin...

MEZA YA MAGAZETI YETU YA LEO ALHAMISI TAREHE 07.04.2016

Image