'Ni vizuri mwanaume, amfiche mkewe vipato vyake’
Ukipata bahati ya kukaa kwenye vijiwe vingi vya wanaume, kauli za ‘mwanamke usimueleze kila kitu’ huwa zinatawala. Wanaambizana kwamba ili uhusiano udumu, usimueleze kila kitu mwanamke. Wanasema mfiche asijue kila kitu. Taswira hiyo imeanza kama utani lakini pengine kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, sasa inakuwa kama sheria. Wanaume wanasambaziana mbinu hiyo ili kukabiliana na wanawake zao. Wanaona ni bora kuwaficha baadhi mambo ili mambo yaende vizuri. Mwanaume anaamini akimficha baadhi ya vitu mkewe, inasaidia kumfanya aishi kwa amani. Hataki kumueleza kila kitu kinachomhusu kwani anaamini uwezo wake wa kukabiliana na mambo hauwezi kuwa sawa na yeye hivyo bora amfiche. Hali hiyo haikuja hivihivi, imetokana na visa mbalimbali wanavyokutana navyo katika uhusiano. Wanafikia hatua ya kuwafananisha wanawake na watoto. Kwamba hata kama mwanaume hana fedha, hapaswi kumueleza mwanamke kuwa hana fedha. Kwamba mwanamke usimueleze vyanzo vy...