STAA AGNES GERALD WAYA APANDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU,AACHIWA KWA DHAMANA
Mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange au Deal (28), amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kutumia dawa za kulevya. Mrembo huyo anayeishi Makongo Juu ambaye alikuwa akitumia muda mwingi kujiziba sura yake kwa mtandio na miwani ya Giza alisomewa tuhuma zake mbele ya Hakimu Mkazi Willbard Mashauri. Hata hivyo, ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama. Mahakama ilimtaka Masogange kuwekwa dhamana ya milioni kumi hali kadhalika na wadhamini wake wawili nao walitakiwa kuwekwa kiasi hicho cha fedha. Aidha mahakama imemuamuru kutosafiri nje ya Dar ea Salaam bila ya kupata kibali cha Mahakama. Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali, Constantine Kakula amedai kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu katika Eneo na Wilaya isiyojulikana lakini ndani ya jiji la Dar es salaam, Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Di...