Jaji Warioba ashauri Viongozi wakutane na Wazungumze
Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba amewataka viongozi wa kisiasa kujenga utamaduni wa kukutana wanapogundua kuna matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani. Jaji Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amesema waasisi wa Taifa walijenga umoja na misingi ya maendeleo ambayo kuna dalili ya kutoweka. Amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 26,2017 jijini Dar es Salaam akifungua mdahalo wa mashauriano juu ya kuhamasisha, kusisitiza, kulinda na kudumisha amani, umoja na maridhiano nchini. Amesema viongozi wa dini wamekuwa na kawaida ya kukutana wanapoona mambo hayaendi sawa jambo ambalo ni zuri na linapaswa kuendelea. Jaji Warioba amesema kuna viashiria vya kutoweka kwa amani na viongozi wa kiserikali na kisiasa wanapaswa kuiga kile wanachofanya wenzao wa dini. "Amani ikitoweka kuirudisha ni shida au kuiendeleza. Viongozi hasa hawa wa kisiasa wawe wepesi kukutana na kuzungumza, tuache malumbano na hasa viongozi wa kisiasa ...