Posts

Showing posts from March 1, 2016

Polisi Yaua Majambazi Watatu....Baada ya Kupekuliwa Walikutwa na Ujumbe wa Kamanda Suleiman Kova

Image
Watu watatu wanaosadikiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi na ujambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi. Watu hao walikutwa na karatasi yenye ujumbe kwa aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ulioandikwa: “Nasaha kwa Kova, mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe.” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jana kuwa tukio hilo, lilitokea Jumamosi iliyopita, eneo la Fire, jijini Arusha wakati mtuhumiwa Athumani Kassim alipokamatwa eneo la Engosheraton akiwa na silaha na aliwataja wenzake. Kamanda Sabas alisema walipopata taarifa kutoka kwa raia wema walio tilia shaka mwenendo wa mtuhumiwa huyo ambaye alipokamatwa, alikutwa na milipuko, makoti makubwa mawili na kofia ya kuficha uso. “Baada ya mahojiano, alituambia kuna wenzake wawili anashirikiana nao kufanya uhalifu na tuliweka mtego. “Saa 5 usiku, askari wetu wakiwa wameambatana na Kassim, walipofika jirani ka...

MBUNGE WA KAWE HALIMA MDEE ATUPWA RUMANDE

Image
  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za shambulio la mwili kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam,  Theresia Mbando. M bunge huyo alinyimwa dhamana na kutupwa rumande. (Picha na Francis Dande) Halima Mdee (katikati) akiwa na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya (wa pili kushoto) pamoja na wafuasi wa Chadema wakati akielekea mahabusu.    Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akisindikizwa na Ofisa wa Polisi, nyumba yake aliyeshika faili kuelekea mahabusu baada ya kunyimwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam. Mwanasheria wa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Prof. Abdallah Safari ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya mbunge huyo kunyimwa dhamana

POLISI WAZIMA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA KILICHOKUWA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU JOSEPH TAWI LA SONGEA

Image
Mmoja wa vijana ambaye anasadikiwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuhamasisha maandamano ya wanafunzi wa vyuo vya Mtakatifu Joseph vya Tawi la Songea vilivyofungwa na serikali  akiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha kuzuia fujo FFU kutokana na kufanya maandamano kinyume cha utaratibu wakitaka kwenda kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati walipodhibitiwa maeneo ya shule ya Bunge posta wakielekea wizarani leo. TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilifuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Baadhi ya askari wakijiandaa kuzuia maandamano ya wanafunzi hao leo maeneo ya wizara ya Fedha na Mipango Posta  jijini Dar es salaam. Wanafunzi hao wakifurumushwa na polisi mara baada ya kuktwa wakia...

HARMONIZE AUFUNGA MWEZI WA PILI NA BADO KAMSHIRIKISHA DIAMOND PLATNUMZ.

Image
Dar es Salaam, Tanzania – February 29, 2016: Mwimbaji anaekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) kutoka Tanzania anayewakilisha kundi la Wasafi Classic Baby( Wcb ),Harmonize ameachia wimbo wake wimbo mpya unaoitwa ‘BADO’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz. SABABU YA KUREKODI WIMBO HUU. Kwa singo mbili alizosikika Harmonize(Aiyola,Kidonda Changu) kwenye vyombo vya habari,jamii imekua ikimfananisha sana na Diamond kwenye uimbaji,ndipo siku moja Harmonize wakati akiimba Diamond alivutiwa na Melody ya wimbo huu na kusema hii itakua nafasi ya Watanzania kuwatofautisha kwenye uimbaji. KUHUSU WIMBO WA BADO. Harmonize alikaa na Diamond akamuuliza ni msichana gani alishamuumiza kiasi kwamba hawezi kumsahau,ingawa Diamond hakumwambia ni msichana gani,lakini akamwambia hiyo ni idea(Mwanga) mzuri wa kutunga wimbo ‘mkali’ Beat ya wimbo huu imetengenezwa na Mtayarishaji(Producer) anaitwa Fraga na kabla ya kurekodi kwenye studio ya Wasafi,producer Fraga alimtumi...

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA MTWARA

Image
Waziri Mkuu, Kassim majliwa akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia) baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016.  Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafany...