Posts

Showing posts from October 1, 2013

BOKO HARAM Lavamia chuo cha kilimo na kuua WANACHUO 50 wakiwa wamelala

Image
Mamlaka nchini Nigeria zimesema kuwa hakukuwa na ulinzi katika chuo cha Kilimo ambako wanafunzi 50 waliuawa kwa kupigwa risasi wakiwa wamelala. Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya tukio hilo lililotekelezwa na wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wenye itikadi kali ya Kiislam wa kundi la Boko Haram katika chuo hicho katika jimbo la Yobe Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Ofisa mmoja wa serikali amesema, serikali na jeshi la wataimarisha ulinzi kwenye maeneo ya shule na kuongeza kuwa licha ya shambulio hilo masomo yataendelea kama kawaida.

UPDATE"mbunge Godbless Lema afutiliwa kesi ya UCHOCHEZI iliyokuwa inamkabili "

Image
Kesi iliyokua inamkabili Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema dhidi ya Mkuu wa Mkoa kwa kusababisha fujo Chuo cha Uhasibu Arusha imefutiliwa mbali na Mahakama kuu muda huu. TUTAKUJUZA HABARI ZAIDI BAADAE .  

Mama ajifungua CHURA...Yadaiwa kuwa mbegu za uzazi wa chura alizipata akioga katika bwawa lenye vyura

Image
Mama mmoja nchini Kenya amejifungua mtoto wa ajabu ambaye anafanana na viumbe wawili wa dunia hii... Sehemu ya juu ya mtoto huyo inafana na chura huku sehemu ya chini ikifanana na binadamu wa kawaida.... Mtoto huyo ambaye alizaliwa wikiendi iliyopita anaonekana kutokuwa na shingo huku macho yake yakiwa kama ya chura. Ripoti ya kitaalamu toka hospitali ya Gaurishnkar ambako mtoto huyo alizaliwa imeeleza kuwa mama huyo aliingiliwa na mbegu za uzazi wa chura wakati akioga katika bwawa la maji.. "Tulifanya mazungungumzo na huyu mama na akatueleza kuwa alikuwa na mazoea ya kuoga katika bwawa.Tunaamini kwamba mbegu za chura zitakuwa zilimwingia wakati akiwa katika siku hatari"..Alisema dakatari mmoja

MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI.... NI UKATILI WA AJABU KWA KICHANGA

Image
  Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni. Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo. Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa. Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo. Rukia Haruna (31) akitolewa nje na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu 218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.