RAY C NAYE ATESWA NA UGUMBA
Nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C. WAKATI staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akiweka wazi kuwa hawezi kupata ujauzito huku Judith Wambura ‘Jide’ naye akisumbuliwa na tatizo hilo, nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C amefunguka na kusema kuwa hali ya kukosa mtoto ambayo ni sawa na ugumba, inamtesa, kwani katika umri wake wa miaka 33, hajabahatika kuwa naye. Akizungumza juzikati, Ray C alisema kuwa pamoja na hamu yake ya muda mrefu ya kupata mtoto, lakini ameshindwa ingawa anaamini siku yoyote Mungu atamuwezesha jambo hilo.“Hao kina Jide, Wema mi naona kama ni cha mtoto. Katika uhusiano wangu wa kimapenzi tangu nivunje ungo, nimewahi kushika mimba mara moja tu, wakati huo nikiwa na Mwisho Mwampamba, lakini bahati mbaya ilitoka, tokea hapo sijapata tena,” alisema staa huyo ambaye yupo katika mapambano ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Alisema katika umri wake huo anatamani sana kuwa na mtoto, kwani wasichana aliozaliwa nao wakati mmoja hivi sasa wan...