Posts

Showing posts from February 7, 2018

Madiwani watatu Chadema wahamia CCM

Image
 Chadema katika Halmashauri ya Tunduma, wilaya ya Momba mkoani Mbeya kimepata pigo baada ya madiwani wake watatu kuhamia CCM. Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Ayub Mlimba (Mwaka Kati), Simon Mbukwa (Kaloleni) na Amos Nzunda (Mpemba) na walitambulishwa jana mchana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Jumaa Irando. Wakizungumza na Mwananchi madiwani hao waliohamia CCM wamesema wamechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza mwelekeo Tunduma, huku viongozi wake wakitoa amri za kibabe wakitaka wanachama kutozungumza chochote. “Unajua baraza la madiwani Tunduma linaundwa na Chadema, sasa tunapewa maagizo ya nini cha kuzungumza na kusimamia hata kama hayaendani na mahitaji ya wananchi wetu kwa lengo tu la watu wachache ndani ya chama,” alisema Nzunda. Mlimba alisema sababu ya kuhamia CCM ni kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli huku Mbukwa akieleza sababu yake kuondoa Chadema kuwa ni mvutano na mtafar...

JPM Azindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi

Image
RAIS Dkt. Magufuli leo  Februari6,  2018 amezindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi (Comprehensive Training Center – CTC) kilichopo Mapinga katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani na kusema amesikia kilio cha wananchi wa Mpinga. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 67.87 na kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa yatakayowawezesha askari kukabiliana na vitisho vya kisasa vya kiusalama. Baada ya uzinduzi huo Rais Magufuli aliweza kupata nafasi ya kuongea na wananchi wa eneo hilo na kusema amesikia kilio chao. “Nimesikia kilio chenu nataka niwahakikishie kwamba daraja hili ni muhimu, si muhimu tu kwa ajili ya kituo hiki bali ni muhimu pia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wanaokaa maeneo haya ninauhakika daraja hili kama litatengenezwa litapunguza gharama za ukaaji huku lakini pia litaweza kutumika kama ‘altenative route’ ikitokea siku moja daraja likakatika Mpigi pale j...

Msukuma Amtolea Povu la Mwaka Waziri wa JPM

Image
MBUNGE na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemshambulia kwa maneno Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina juu ya ‘operation’ anazozifanya za kionevu za kupambana na uvuvi haramu kwa kumwambia aache kufanya kazi kwa mihemuko. Msukuma ameeleza hayo katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati akichangia uwasilishaji wa kamati ya kudumu ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji baada ya kupita miezi kadhaa tokea Waziri Mpina kutoa kauli yake kuachia madaraka endapo tatizo la uvuvi haramu litaendelea kuwa sugu nchini jambo ambalo kwa sasa Msukuma anadai kiongozi huyo analifanya bila ya kufuata sheria zilizopo kwa kuzuia watu wasivue dagaa na kupelekea kuwapa athari wananchi wanyonge na kumuomba aundiwe tume ya uchunguzi yeye timu yake. “Toka nazaliwa sijawahi kuona sheria hizi zinazotumiwa na Waziri wa Mifugo Mpina, umri wangu huu nimeshuhudia awamu zote za Mawaziri. Nafikilia kwamba ndio tunaanza kutunga sheria au h...