Mtoto wa zari amliza Diamond.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul āDiamond Platnumzā, akiwa na mtoto wake P rincess Tiffah . Musa mateja na imelda mtema HII ni kali! Muda mchache baada ya mwandani wake, Zarinah Hassan āZari The Boss Ladyā kujifungua salama, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul āDiamond Platnumzā, amejifungia chemba kisha kuangua kilio akisema Mungu ni mwema huku akiwataja waliowahi kuwa wapenzi wake, Penniel Mungilwa āPennyā na Jokate Mwegelo kwa maneno yao ya shombo. Mama yake Diamond Platnumz, Sanura Kassim āSandraā akiwa na mjukuu wake wakiwa na Zari baada ya kujifungua. TUJIUNGE AGA KHAN Tukio la kujifungua mchumba wa Diamond, Zari lilijiri Agosti 6, mwaka huu mishale ya saa 10:40 alfajiri katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar ambapo alipelekwa usiku huo baada ya kujisikia uchungu ambapo alijifungua mtoto huyo wa kike. Chanzo cha habari kilieleza kwamba, siku hiyo, wakiwa hospitalini hapo, muda mfupi tu baada ya Diamond kuambiwa kuwa tayari Zari amejifungua, ...