MHASIBU UBALOZI WA TANZANIA MSUMBIJI APANDISHWA KORTINI KISUTU
Mhasibu Joyce Moshi akishuka ngazi za mahakama baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili. MHASIBU wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi (56) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka tisa ikiwemo ya utakatishaji fedha wa dola za Marekani 150,000. Moshi ambaye ni Mkazi wa Temeke alifikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Wakili wa Serikali, Saimon Wankyo alidai kuwa Oktoba 25, 2016 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Maputo nchini Msumbiji, alighushi barua ikionesha kwamba Ubalozi wa Tanzania Nchini Msumbiji Umeielekeza Benki ya MIllenium kupeleka Dola za kimarekani elfu kumi katika akaunti inayomilikiwa na Joyce Moshi akijua yakuwa siyo kweli. Inadaiwa barua hiyo ilionyesha kuwa ubalozi umeelekeza Benki ya ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa ...