Posts

Showing posts from November 22, 2017

NAIBU WAZIRI MASAUNI, KAMISHNA JENERALI WAKAGUA MPAKA WA TANZANIA KENYA ULIOPO WILAYANI TARIME

Image
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) wakiangalia jiwe la mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda, wilayani Tarime ambapo upande wa pili ni Kaunti ya Migori nchini Kenya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua mipaka na kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu kupitia vipenyo katika mipaka hiyo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea alama ya Mpaka unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya uliopo katika kijiji cha Nyamhunda wilayani Tarime.Wengine ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk, Anna Makakala, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua m...

NANDY ATOA YA MOYONI,AFUNGUKA TENA KUHUSU KUPENDA

Image
MWANA-DADA anayefanya vizuri katika Bongo Fleva Faustina Charles ‘Nandy’ ameeleza kuwa hampendi mwanaume kwa sababu ya mkwanja isipokuwa anataka mapenzi ya kweli. Akipiga stori na Risasi Vibes, Nandy ambaye anatamba na ngoma ya Kivuruge alisema anachopenda yeye ni mwanaume mcha Mungu na mchapakazi, haijalishi kama hiyo kazi inamuingizia kipato kikubwa au la. “Fedha siyo kigezo cha mwanaume kuwa na mimi, muhimu mtu awe na hofu ya Mungu, asiwe mtu wa kujibweteka awe anajish-ughulisha kwa kazi yoyote ile, tutapambana wote kutafuta maisha hadi mambo yatakapokuwa vizuri na kujivunia kwa pamoja,”alisema. STORI: MAYASA MARIWATA | GLOBAL PUBLISHERS

Jide, FA Wanaurudisha Muziki wa Bongo Juu

Image
Judith Mbibo Wambura. KAMA ilivyokuwa wakati walipotibuana, kwamba watu wachache walio karibu yao ndiyo waliojua chanzo, ndivyo inavyotokea tena sasa hivi inapofahamika kuwa bifu baina yao limeisha. Nawazungumzia ma-legend wawili katika Bongo Fleva, Judith Mbibo Wambura ambaye wengi tunamfahamu kama Lady Jaydee na Hamis Mwinjuma, hapa akifahamika zaidi kama Mwana FA. Na watu wasingejua kirahisi kama wawili hawa wako kwenye ugomvi kama siyo wote wawili kutangaza kufanya shoo kwa siku moja. Jide alikuwa na onyesho lake la kutimiza miaka 13 katika Bongo Fleva ambayo ilipangwa kufanyika pale Nyumbani Lounge huku Mwana FA, akiitangaza siku hiyo kuwa na onyesho alilolipa jina la The Finest, ambalo lilipangwa kupigwa katika viwanja vya Makumbusho, kule Posta, jijini Dar. Hiyo ilikuwa ni Mei 2013. Mwana FA. Shoo zao hizo zilikuwa zipigwe Mei 31, 2013 lakini ghafla likaibuka tukio kubwa Bongo Fleva, baada ya taarifa kuwa rapa mkali, bingwa wa freestyle Bongo, ...

RC Makonda Atembelea Ofisi za Clouds Media Group Kutoa Pole

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,  Paul Makonda (wa pili kulia),  akinena jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga (kushoto). MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es Salaam mapema leo ametembelea Ofisi za Clouds Media Group kutoa pole ikiwa ni siku moja baada ya ofisi hizo kukumbwa na janga la moto uliotokea hapo jana majira ya saa nne asubuhi. Makonda akiongea na maofisa wa vikosi vya usalama. Viongozi wengine wa serikali waliofika ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Ally Hapi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta. Hata hivyo, tayari matangazo ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV yamerejea hewani baada ya kupotea siku nzima  jana kutokana na hitilafu ya iliyosababishwa na moto huo ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMJULIA HALI MZEE ABDULRAZACK MUSSA SIMAI ‘KWACHA’ ALIYELAZWA MOI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo alimtembelea na kumjulia hali Mzee Abdulrazack Mussa Simai ‘Kwacha’ ambaye amelazwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).Mzee Abdulrazack Mussa Simai ‘Kwacha’ ni Mzee wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia alishawahi shika nafasi mbali mbali za Uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Post Views: 50