Posts

Showing posts from April 24, 2017

Steve Nyerere aporomosha jambo lingine leo

Image
Muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Steve  Nyerere amemuombea msamaha msanii wa muziki Nay wa Mitego kwa kuwaita wasanii wa filamu wote walioandamana kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje ya nchi kuwa ni 'Matahira' Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Steve Nyerere amesema kwamba yawezekana  Nay wa Mitego alikuwa na hasira hivyo akashindwa kutumia lugha sahihi ya kuwaelekeza wasanii wenzake walivyokuwa wanakosea ndio maana alitoa lugha yenye maneno makali ijapokuwa alikuwa sahihi kukosoa maandamano yale. "Kwanza naomba nimuombee msamaha ndugu yangu Nay wa Mitego, hakuwa na nia mbaya lakini hakutumia maadili kufikisha ujumbe wake, Unajua sisi watanzania hatupendi kuambiwa ukweli na hata tukisemana tuna lugha zetu laini za kusemeshana. Nay wa Mitego mpaka kutoa maneno makali vile ujue anaipenda tasnia yetu ya filamu alikuwa kaaumia, si unajua hata yeye alishawahi kuwa huku anatuonea huruma na anatupenda mimi niseme

Kambi ya Upinzani Walivyogoma Kusoma Hotuba Yao Bungeni

Image
Msemaji wa upinzani katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Ally Salehe amesusa kusoma hotuba yake ya upinzani kuhusu wizara hiyo baada ya kuamriwa kuacha kusoma baadhi ya maneno yakiwamo yanayohusu Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar na mgogoro wa CUF. Hali  hiyo imetokea bungeni leo Jumatatu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju kusimama na kupinga baadhi ya maneneo aliyotumia kama  “Kila wizara imekiona cha moto, wamebanwa mpaka wamevunjwa mbavu” na kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeathirika vibaya na kisu cha ngariba kwa kukata bajeti yake. Baada ya malumbano, Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu alitoa uamuzi kuwa maneno yaliyoandikwa kuanzia ukurasa wa tatu hadi wa saba kwenye hotuba hiyo yasisomwe wala kurekodiwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge. Baada ya uamuzi huo, Salehe alisema basi asingeendelea kuisoma hotuba yake na yaliyobaki anamwachia ‘ngariba’ afanye anavyotaka.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Abdallah Bulembo mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya k

Rais Magufuli amefanya uteuzi huu leo April 24

Image
Rais Dkt @MagufuliJP amemteua Prof. Chibunda kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Mmarekani aliyekamatwa Korea Kaskazini atambuliwa

Image
Bw Kim amekuwa akifunza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST) Chuo kikuu kimoja nchini Korea Kaskazini kimesema raia wa Marekani aliyekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa nchi hiyo Jumamosi alikuwa mhadhiri katika chuo hicho. Wamesema jina lake ni Kim Sang-duk, lakini pia amekuwa akifahamika kamaTony Kim. Mhadhiri huyo ambaye ni Mmarekani wa asili ya Korea amekuwa akifunza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST) kwa wiki kadha kabla ya kukamatwa kwake. Chuo kikuu hicho hata hivyo kimesema masuala yaliyopelekea kukamatwa kwa Bw Kim hayana uhusiano wowote na chuo hicho. Bw Kim alikamatwa alipokuwa anajiandaa kuondoka Pyongyang. Maafisa wa Korea Kaskazini bado hawajasema sababu iliyochangia kukamatwa kwake. Shirika la habari la Korea Kusini Yonhap limesema Bw Kim, ambaye umri wake ni miaka hamsini hivi, alikuwa anashiriki katika mipango ya kutoa misaada na alikuwa Korea Kaskazini kufanya mashauriano

NGORONGORO KITOVU CHA UTALII KINACHOWAVUTIA WATU MASHUHURI DUNIANI

Image
Na Jumia Travel Tanzania Inaonekana mwaka 2017 umeanza vizuri katika sekta ya utalii nchini Tanzania kutokana na watu kadhaa mashuhuri kuzuru vivutio vyake. Sehemu ambazo zimeonekana kuwavutia watu wengi zaidi ni hifadhi ya mbuga ya Serengeti na bonde la Ngorongoro. Alianza mwigizaji maarufu wa filamu kutokea Hollywood nchini Marekani, Will Smith na mkewe Jada Pinkett-Smith. Mwanzoni mwa mwezi Machi walitua nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kujivinjari katika mbuga ya Serengeti. Wakiwa huko familia ya Smith walikutana na msanii mwingine kutokea huko huko Marekani, lakini huyu yeye ni mwanamitindo na mrembo, Chanel Iman. Haikupita muda mrefu sana tangu watu hao mashuhuri kuwepo nchini, kwani siku chache zilizopita aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Taifa la Israel, Bw. Ehud Barak naye alitembelea mbuga ya Serengeti pamoja na Ngorongoro. Hii ni ishara nzuri kwa sekta ya utalii nchini ambapo kupitia watu hawa maarufu wen

MFANYABIASHARA Achomwa Visu 14 na Kaka’ke..!!!

Image
 Mfanyabiashara wa samaki, Warioba Mtatiro, mkazi wa Kijiji cha Etalo, Musoma Vijijini, amedaiwa kujeruhiwa vibaya kwa kisu na kaka yake (jina tunalihifadhi). Tukio hilo la kusikitisha limetokea hivi karibuni katika Mtaa wa Nyamulinda, Kijiji cha Etalo, Musoma Vijijini. Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mtiti huo, Mtatiro alikuwa akicheza kamari maarufu mkoani Mara kwa jina la Magaramka na kaka yake ndiye aliyekuwa akichezesha. Alisema baada ya ‘kupunwa’, Mtatiro hakuwa na kiasi hicho cha fedha kilichohitajika katika mchezo huo ndipo ugomvi ukaibuka hadi kufikia hatua ya kaka kumchoma visu mdogo wake. “Mtatiro alipunwa shilingi mia tano. Sasa kaka yake akawa anamdai na yeye akawa hana ndipo alipoamua kuchukua kisu na kuanza kumchoma. “Alimchoma sehemu mbalimbali mwilini, kichwani na mgongoni na kumsababishia majeraha makubwa. Kwani alikuwa anachoma kisha anachomoa na kuchoma sehemu nyingine kama mara 14,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilieleza kuwa, baa

Studio Aliyotekewa Roma na Wenzake Yafungwa

Image
Roma Mkatoliki na mwanaye Ivan. DAR ES SALAAM: Zikiwa zimepita wiki kadhaa tangu staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ na wenzake watatu, Moni, Imma na Bin Laden walipotekwa wakiwa kwenye Studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki, Dar na kupatikana baada ya siku tatu wakiwa na majeraha, habari mpya ni kwamba studio hiyo imefungwa na haifanyi kazi kwa sasa. Wikienda lilifika kwenye studio hiyo na kuzungumza na chanzo kilichokutwa jirani yake ambapo kilieleza kwamba, tangu alipotekwa Roma na wenzake wakiwa ndani ya studio hiyo huku kompyuta na TV vikichukuliwa na watekaji hao, studio hiyo haijawahi kufunguliwa na haijulikani itafunguliwa lini kwani bado hofu ni kubwa. “Hofu ni kubwa sana tangu utekaji ufanyike, imebidi studio ifungwe na haijulikani itakuwa wazi lini, ukizingatia waliotekwa bado wako nyumbani wanauguza majeraha waliyoyapata na hali zao bado siyo nzuri hasa Roma,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kupata habari hizo,

Ishu ya Bongo Muvi Kuandamana… Nay wa Mitego, Mlela Hapatoshi

Image
BAADA ya wiki iliyopita mastaa wa filamu kuandamana kupinga uuzaji holela wa filamu za nje ya nchi kwa sababu zinawaharibia soko, hali imekuwa tete kwa msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na muigizaji Yusuf Mlela kutokana na kutoleana maneno makali, Wikienda lina data kamili. Akizungumza na Wikienda, Nay alisema anawashangaa wasanii wa filamu kuandamana kisa filamu za nje wakati zilianza kuuzwa hata kabla wao hawajafikiria kuanza kuigiza hivyo wanatakiwa kufanya kazi nzuri zenye ubunifu na siyo vinginevyo. “Nawashangaa sana Bongo Muvi kuandamana, muvi za nje zipo tangu enzi na enzi hata kabla wao hawajaingia kwenye sanaa hiyo, wanatakiwa kufanya kazi maana wamekosa ubunifu pia waache upuuzi,” alisema Nay. Baada ya Nay kuzungumza hayo Mlela naye alimjibu kwa kumwambia kwamba anatakiwa kukaa kimya kwani wanachofanya wanatetea haki yao kwani Nay alikuwa chokoraa tu lakini sasa amefanikiwa ndiyo anaongea maneno yasiyofaa kwa ku

Jokate aivuruga UVCCM ni baada ya kuteuliwa

Image
UTEUZI wa Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, unaonekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo. Mjadala mkubwa umeibuka kuhusu uteuzi huo, ambapo baadhi ya wanachama na viongozi wa juu wa jumuiya hiyo wamedai kuwa haukufuata kanuni na taratibu za umoja huo. Vyanzo vya kuaminika kutoka katika umoja huo vimeliambia MTANZANIA kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa UVCCM hawakushirikishwa katika uteuzi huo uliofanywa na kigogo mmoja wa umoja huo. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa uteuzi huo haukushirikisha wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wala Baraza Kuu la UVCCM, ambalo halikukutana kumthibitisha Jokate kama kanuni zinavyoelekeza. Kwa mujibu wa kanuni za jumuiya hiyo, wajumbe wa kamati ya utekelezaji hawazidi 10, ambapo miongoni mwao ni Mwenyekiti wa umoja huo Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na mjumbe mmoja kutoka makao ma

NAPE NNAUYE ATOA NENO HILI KUHUSU VURUGU ZA CUF

Image
Kufuatia watu wanane kuibuka wakiwa na silaha na kusababisha vurugu kwenye mkutano wa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya kinondoni, Dar, Jumamosi iliyopita, Mbunge wa Mtama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Moses Nnauye ametia neno kwa kusema kuwa hizo ni siasa za kinung’ayembe. Vurugu za CUF juzi Jumamosi. Jana Nape aliandika kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter:  “Siasa ni ushindani wa hoja na siyo nguvu! Tunakwenda wapi huku jamani? Wanavamia na kutoroka!!?? How!!? Siasa imevamiwa na manung’anyembe sasa! Tafsiri ya nung’ayembe ni mwanamke asiyeolewa anayehangaika ya maisha ya kurukaruka. Tukio la kufanyiwa fujo mkutano wa CUF lilijiri katika Hoteli ya Niva iliyopo Mabibo, Dar ambapo ilidaiwa kuwa, wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Maalim Seif waliumizwa kwa kupigwa na wavamizi waliodaiwa ni wale wanamuunga mkono Profesa Lipumba. Katika vurugu hizo, pia wandishi wa habari ambao walijitete lakini walishambuliwa ni pamoja na F