RC Mongella ashiriki mazishi ya Bibi yake Paul Makonda


Na James Timber, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella leo Agosti 23, ameungana na waombolezaji mbalimbali kushiriki mazishi ya Bi. Anna Makwega Manasse (81) ambaye ni Bibi wa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda.

Mazishi ya Bi. Manasse ambaye alifariki dunia juzi Agosti 21, Mwaka huu akiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu, yamefanyika katika makaburi ya nyumbani yaliyopo Kahangala wilayani Magu.


Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa serikali mkoani Mwanza, Mkuu wa Mkoa Mongella amewaombea kuwa na uvumilivu kwa  ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo na kuwahimiza kumuombea kwa Mola ili apumzike kwa Amani.

Comments

Popular posts from this blog