Posts

Showing posts from June 6, 2016

RAIS DKT MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA RAIS WA SAHARAWI, AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA UBELGIJI, BALOZI WA MAREKANI NA KUAGANA NA BALOZI WA ITALY

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya Nje wa Ubelgiji Mhe. Didier Reynders aliyemtembelea Ikulu Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italy nchini Mhe. Luigi Scotto  aliyemtembelea na kumuaga baada ya kumaliza muda wale wa kazi Ikulu Dar es salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italy nchini Mhe. Luigi Scotto  aliyemtembelea na kumuaga baada ya kumaliza muda wale wa kazi Ikulu D...

TAARIFA YA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKALA WA UAGIZAJI WA MAFUTA KWA PAMOJA (PBPA)

Image
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb), amemteua Dk. Steve Mdachikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kuanzia tarehe 03 Juni, 2016. Kufuatia uteuzi huo, amewateua pia wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PBPA kuanzia tarehe 03 Juni, 2016. 1. Dkt. Daniel Sabai 2. Dkt. Henry Chalu 3. Dkt. Siasa Mzenzi 4. Mr. Salum Mnuna Imetolewa na; KATIBU MKUU 6 Juni, 2016

TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA KODI KWA MWEZI MEI 2016

Image
MKamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata akitilia mkazo jambo wakati wa kikao na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwezi Mei 2016,kilichofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abdul Mapembe. MAMLAKA ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.032 katika mwezi Mei ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.025 katika mwezi huo. Makusanyo ya kipindi cha miezi kumi na moja (Julai 2015 hadi Mei 2016) ni jumla ya shilingi trilioni 11.956 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la shilingi trilioni 12.054 katika lengo la kipindi hicho kwa Tanzania Bara na Zanzibar. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata amesema TRA inaendelea na jitihada mbalimbali kuhakiki...

MSANII DIAMOND ATOA MSAADA WA MADAWATI 600 KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE. MAKONDA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Mkoa wetu. Akiongea katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika kukabilana na changamoto za elimu. Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ili kuweza kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini. Makabidhiano hayo yalifanyika leo Juni 6, 2016 ofisini kwa mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600 ikiwa ni mchango wake k...

Polisi Jijini Mwanza Wapambana na Majambazi kwa Saa 16, Wakamata Silaha Nzito, Watatu Wauawa

Image
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkia jana jumapili katika mapango ya mlima wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini Mwanza. Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,amewataja majambazi waliouwa katika majibizano ya risasi usiku kucha kuwa ni Omar Francis Kitaleti mkazi wa Nyegezi Kona,said Khamis Mbuli maarufu kama fundi bomba mkazi wa bugarika na jambazi mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika. Amesema majambazi hayo yalikuwa yamejificha kwenye mapango ya mlima wa Utemini kabla ya askari polisi kufanikiwa kuyaua. Jambazi mmoja aliyeuawa ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 25 alikuwa akiwashambulia polisi kwa kutumia bastola ambapo baada ya polisi kumpiga risasi walimpekua na kumkuta akiwa na bastola aina ya Chinese,iliyokuwa na risasi tatu ndani ya magazine,huku majambazi wengine waliokuwepo kwenye mapango hayo wakiendelea kujibishana kwa ...

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA IBADA KATIKA KANISA LA MAOMBEZI LA MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO UBUNGO KIBANGU LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabarainayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside. Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo‘mzee wa upako akiagana na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada yakuhudhuria ibada katika Kanisa la Maombezi Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru waumini wa kanisa hilo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa la Maombezi la Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)