Posts

Showing posts from June 12, 2018

Tabia Ya Kuzoeana inavyoweza kuathiri Maisha yako ya kimahusiano

Image
Kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla. Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini. Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinn...

Breaking News: Madrid Wamtangaza Lopetegui Kuwa Kocha Mpya

Image
Julen Lopetegui Klabu ya Real Madrid imemtangaza Kocha wa sasa wa Hispania, Julen Lopetegui kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo na atajiunga nayo baada ya mashindano ya Kombe la Dunia

Nape Nnauye: Bora mnilaumu kwa 'Bao la mkono' sio kwa hili la Jamii Forums

Image
Mbunge Mtama, Nape Nnauye amejikutaka akijibu hoja mbali mbali mtandaoni kufuatia mtandao wa Jamii Forums kusitisha kutoa huduma. Utakumbuka Jamii Forums wamefikia hatua hiyo kutokana na kanuni za maudhui ya kimtandao za mwaka 2018. Sasa Nape Nnaye alianza kueleza hisia zake kuhusu hilo kwa kuandika kwenye mtandao wa twitter; Hili la JF linafikirisha! Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza Kutana nao….. kimya kimya!. Baada ya tweet hiyo idadi kubwa ya wachangia walionekana kuomnyooshea kutokana kipindi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipitisha sheria ya huduma za vyombo vya habari kwa mwaka 2016 Hata hivyo Nape aliwataka wachangia kutofautisha vitu hivyo kwani ni sheria mbili tofauti. “Nimeuliza hili swali toka mwanzo kina uhusiano gani wa hizi sheria mbili? Au tunakaririshwa au hatujui tunachotaka kusema,” alijibu Nape na mjadala kuendelea. Utakumbuka katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 2015 wakati Nape Nnaye akiwa Katibu Mwenezi ...

JPM Amwaga Tsh. Milioni 10 Cash Ujenzi wa Msikiti Dar

Image
RAIS John Magufuli ametoa pesa taslim kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mifuko 625 ya sementi itakayosaidi kwenye ujenzi wa Msikiti Mkuu wa BAKWATA unaoendelea kujengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Rais ametoa mchango huo leo Juni 12, 2018 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti huo unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco. Msikiti huo ambao utakuwa mkubwa kuliko misikiti yote nchini Tanzania utabeba zaidi ya watu 8,000 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili au mei mwakani. “Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote,” amesema Rais Magufuli

UKWELI KUHUSU WANAFUNZI UDSM WALIOFARIKI DUNIA AJALINI

Image
TAARIFA zinazosambaa mitandaoni zikisema mwanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Maria Godian Soko amefariki dunia kwa ajali usiku wa kuamkia leo maeneo ya Ubungo Riverside, Dar es Salaam, akiwa anakimbizwa hospitali kwa matatizo ya ujauzito, zimekanushwa na Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika chuo hicho, Hussein Amri Aman, aliyesema kwamba kwamba marehemu hakuwa na tatizo hilo. Amri amesema  marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu kwa muda mrefu,  hali iliyokuwa ikisababisha apoteze fahamu, na ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe anakimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa (ambulance). “ Marehemu Maria alikuwa na matatizo ya pumu ambayo yalimsababishia kifua kubana hadi kuzimia, majira ya saa mbili kasoro usiku tulifanya utaratibu wa kuita ambulance ya chuo na kumchukua hapa Mabibo hostel kumpeleka hospitali ya chuo kwa matibabu zaidi” Ameongeza: “ Wakati taratibu za kumpeleka ...

Historia Imeandikwa: Trump, Kim Jong Un Wakutana Live Singapore

Image
MKUTANO  wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani,  Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini,  Kim Jong Un,  umefanyika nchini Singapore. Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili  pekee yao na wakalimani wao. Mkutano huo ulianza kwa viongozi  hao wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao. Rais Trump amesema wawili hao wamepiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka za makubaliano. Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama katika rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia. Hata hivyo, haijabainika ni nini kitakuwepo kwenye waraka ambao watautia saini. Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kuf...

Kafulila kuelezea sakata la Tegeta Escrow

Image
Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema ataanza kuelezea kwa kina sakata lililotikisa nchi la kashfa ya Tegeta Escrow wiki ijayo kupitia gazeti la Uwazi. Akizungmza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, Kafulila alisema amegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo wananchi wanataka kuyajua kuhusu sakata hilo, hivyo ameamua kuyaandika yote ili kiu ya Watanzania kujua kuhusu sakata hilo iishe. “Najua kwamba mimi ndiye niliyelibebea bango bungeni sakata lile na kwa kuwa Gazeti la Uwazi linasomwa na watu wengi, nimeamua kuyaeleza yote kupitia gazeti hili kuanzia toleo lijalo,” alisema Kafulila. Alifafanua kuwa wazo la kuandika sakata hilo amelipata baada ya kuulizwa sana na baadhi ya wananchi kwamba liliishaje na jinsi lilivyomfanya akorofishane na vigogo wengi na hata kujihatarishia maisha. “Kwa kuwa hilo ni jambo zito, ni vema wananchi wajiandae kusoma kwa urefu juu ya sakata hilo kwenye gazeti hili. Nadhani nimefanya uamuzi sahihi,” alisema Kafulila. ...

Ulinzi wa Rais wa Korea Kaskazini usipime

Image
Ulimwengu kwa mara nyengine ulipata fursa ya kuwatazama walinzi 12 wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un wakikimbia wakati walipokuwa wakiulinda msafara wake nchini Singapore. Lakini wana majukumu mengi kwa sababu linapojiri swala la usalama wa kiongozi huyo, taifa la Korea liko tayari kufanya chochote . Mchanganuzi Michael Madden anaelezea zaidi kuhusu kundi hili la wanaume. Wakati anapokuwa Korea Kaskazini , mlinzi wa karibu wa Kim ana laini tatu tofauti zinazomzunguka. Walinzi wanaokimbia kandokando ya gari lake aina ya Limousine na wale wanaotembea kwa mguu ni miongoni mwa maafisa wa afisi kwa jina Central Party Office #6, inayojulikana rasmi kuwa afisi ya wapiganaji. Wao ndio wanaomlinda rais huyo na huchaguliwa kutoka katika jeshi la Korea. Huchaguliwa kutokana na vigezo vya , urefu-wanatakiwa kuwa na urefu sawa na kiongozi wao na wawe wanaweza kuona vizuri. Wanatakiwa kuwa na uwezo kama vile kupiga risasi na kupigana judo, karate na masumbwi. Mwisho...